Msaada wa chakula cha mtoto

Double K

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
907
Reaction score
342
Habari wana jf,

nina mtoto mchanga nilikuwa namnyonyesha tu, sasa ni miezi mitano na nimeanza kazi nahisi maziwa yangu pekeyake hayamtoshi hashibi. nilianza kumpa maziwa ya SMA ila anaharisha sijui ni mwanzo au nifanyeje. naomba anayejua lishe au chakula cha kumpa ili nianze kumpa. asanteni.
 
anza na maziwa ya ng'ombe,maziwa yakiwa nusu kikombe ongeza na maji nusu kikombe yachemke vizuri na utumie vyombo vyake special na vichemshwe kwa uoshaji.
 
huo ni mchakamchaka!!

mwanangu alikataa kunyonya akiwa na miezi 2. Nilikomajee!!! Kila nikimpa maziwa ya kopo anaharisha...

kakuzwa na maziwa ya ng'ombe tu mpk akipofikisha miezi 5 ndipo nilipoanza kumpa uji wa dona, alipoanza wa 7 nikaanza kumpa uji wa lishe niliopikia maziwa bila kuacha maziwa na vijuice kimtindo! viugali kwa mbali, mara vimtori, mara visupu vya samaki, na mbogamboga, jana katimiza miezi 8 ana kilo za kutosha kbs, anaafya nzuri na anavutia machoni pa watu.

Namshukuru Mungu hajawahi kuugua kivile japo waliniambia mtoto ambae hajanyonya ni hekalu la magonjwa.

Nimejifunza mengi kupitia mitandao, jinsi ya kumtengenezea chakula, jinsi ya kumtengenezea uji wake wa lishe,kumlisha matunda na vitu vingi.

leo naitwa mama Bonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…