Fungus katika ya vidole ni fungus ya kawaida inawezekana wewe mtumiaji sana wa maji, kwani maji huchimbua mwili!! kwahivo vijidudu kama hivo huingia na kupambana na white blood cells lakini kwa kuzidiwa nguvu ndio fungus hujitokeza, kama fungus uliyoisema wewe ni ya kawaida ila ina kero kwakweli.
Kwanza kabisa kama mtumiaji wa maji sana upunguze yaani sio kutumia maji kwa kunywa laa! kutumia maji yaani kuchezea maji inawezekana ukikoga unatumia maji zaidi au kila wakati unakosha miguu yako na mambo kama hayo. Hata hivo ipo dawa
moja na nafikiri inajulikana sana nayo ni ndimu na jivu. Unachukua jivu unaweka katika sehemu hiyo katikati ya kidole na halafu unanyunyizia ndimu! Dawa nzuri lakini inawasha sana.! Inshallah nafikiri umenifahamu.
Au tafuta Dawa hii Kuna powder inaitwa 'DEODORANT POWDER' "FAA" inapatikana masupermarket, huenda ikawa iko kabila jengine kwani FAA ni sabuni, na hiyo ni powder ambayo pia ni nzuri na inawafaa kwa wale wanaotoka majasho kisha wakatokwa na harufu. Hii powder ukisha kukoga unakuchunja kidole kimoja kimoja na unatia ni uzuri wakati unapokwenda kulala inakausha na pia hutoki harufu ya miguu.
Sababu yake ni kuvaa soksi na boot kwenye nchi za joto ndio hufanya jasho kwenye vidole na kusababisha fungus. kwa hivyo jaribu usikae muda mrefu na soksi na boot au badilisha viatu na usivae soksi.
Au Tafuta Dawa iitwayo Dactarin ambayo ni cream. Hii ni nzuri kutumia mara mwasho unapotokea lakini si iwapo pameshafanya jeraha.
Dawa nyengine ya Fungus ni 'DAKESEN' Prickly Heat Powder - Cooling and Refreshing, inauzwa kwenye masupermarket i . unatia wakati unapokwenda kulala kwa kufungua kidole kimoja kimoja na kutia hiyo powder. InshaAllah kwa uwezo wake Subhana itaondoka.
***HII POWDER NI NZURI SANA PIA KWA WATOTO AU WATU WAZIMA WENYE KUPATA TETE KUANGA UNAKUWA UNAMTUMILIYA MTU KWA KUMPAKA MWILI MZIMA KWA KILA UNAPOKUMBUKA. INAVUNJA NGUVU YA TETE KUANGA NA HAZIENEI NA KUKAUKA KWA HARAKA.