Msaada wa dawa ya kupunguza usingizi

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Wakuu, habari za wakati huu.

Nimekuja kwenu kuomba msaada wa dawa ya kupunguza kulala.

Nalala mapema sana, naweza kulala sa 1, sa 2 au hata sa 12 kama nimewahi kurudi nyumbani.

Nahitaji dawa angalau ya kuniweka macho angalau hadi sa 4 au sa 5 usiku. Hii ya kulala mapema inanikwaza sana. Nilipokua mdogo nilikua naweza kulala hata kuanzia sa 11 jioni. Na nilipokua mdogo zaidi naambiwa nikilala sa 11 jioni nitaamka kesho sa 5 au sa 4 asubuhi, watu walikua wanadhani nimekufa. Sasa hili naona linaniandama hadi sasa. Nilipokua nasoma shule ya bweni, naambiwa nikae prep hadi sa 4 ilinishida, sa 2 tu nishaenda kulala au nalala darasani.

Angawaje nawahi kuamka hata kama nikilala sa 10 ikifika sa 12 lazima niamke ila hii ya kuwahi kulala inaniboa sana.

Naweza kua mahala labda Bar ingawa sinywi pombe kwa ajili ya kubuy time ili nisiwahi kulala ila muda wote nahisi usingizi.

Naombeni msaada wa natural remedies au hata over the counter medications.

Ahsanteni sana.

MREJESHO.

Wakuu, nawashukuruni sana mlionishauri nitumie kahawa.

Kabla sijatoka ofisini sa moja hivi kasoro nikamuomba mama mhudumu wa ofisi aniandalie kikombe cha gawaha ila mara moja zaidi ya kipimo cha kawaida.

Toka nimefika nyumbani sa moja niko sebuleni natazama tv wala sijahisi aina yoyote ya usingizi kitu ambacho sio kawaida kabisa kwangu, ningekua nishalala sebuleni au kuhisi kwenda kulala muda mrefu sana.

Itabidi niweke kahawa kama kinywaji changu rasmi kunywa masaa kadhaa kabla ya kulala ili niwe nakua macho angalau hadi sa 4 au 5.

Ahsanteni sana. Karbuni tuangalie televisheni.
 
Chunguza Kwanza unafanya kazi gani either ni ngumu au kazi za kawaida walahi

Kulala si kuumwa walahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia kahawa kila jioni. Utakaa macho hadi utachukia
 
Simple.

Tumia vitu vyenye caffeine nyingi.

Kuna vidonge kama No Doz.

Pia waweza kunywa kahawa, soda za Pepsi au Coca Cola, na kadhalika.
Soda niliacha kunywa 2013 kwa sababu tu hazina faida mwilini zaidi ya kuongeza sukari.

Ni vitu gani vyenye caffein nyingi mkuu. Na hivyo vidonge vya Na Doz zinafanyaje kazi mkuu.

Ahsante kwa hii tip mkuu.
 
Soda niliacha kunywa 2013 kwa sababu tu hazina faida mwilini zaidi ya kuongeza sukari.

Ni vitu gani vyenye caffein nyingi mkuu. Na hivyo vidonge vya Na Doz zinafanyaje kazi mkuu.

Ahsante kwa hii tip mkuu.

Soda aina ya Pepsi na Coca Cola zina caffeine nyingi sana.

Kahawa ina caffeine nyingi.

Red Bull ina caffeine nyingi.

Vidonge vya No Doz vina caffeine nyingi pia.

Kwa ufupi, caffeine inakusaidia kutokupata usingizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…