Pole kwa matatizo hayo ya macho yanayokusumbua.....
Hivyo bhasi kwanza tufahamu nini maana ya mtoto wa jicho; Hii ni condition ambayo mara nyingi hushambulia lens ya jicho na hivyo hupelekea kutengeneza ukungu (cloudiness) katika lens ya jicho na hivyo kwa hapo baadae ikishindikana kurekebishwa yaweza sababisha upofu.....
Mara nyingi condition hii huathiri au kushambulia cell mbalimbali za lens na hivyo kuzifanya kupoteza maji, kusinyaa na hivyo kupandiana na hivyo kutengeneza ukungu fulani katikati ya lens hivyo jicho kushindwa kuakisi mwanga vilivyo na hivyo hupelekea mtu ambaye ana ugonjwa huu kushindwa kuona vitu vizuri.....
Vifuatavyo vyaweza sababisha mtoto wa jicho; Yaweza kuwa ya kurithiwa, Yaweza kumtokea mtu mwenye kisukari, upungufu wa calcium (Hypocalcium), kuwa na lishe mbovu, Kuharibiwa kwa layer ya katikati ambayo hutenganisha retina ya jicho na sclera hizo ni baadhi tu....
Upimaji wa macho ili kuweza kubaini tatizo ni kwa kutumia kifaa kinachoitwa
ophalmoscopy kujua response ya jicho kwa mwanga na
pia kulichunguza jicho kwa ukaribu kubaini kama lina tatizo kwa kujaribu kama kuligusa na lisipojaribu kufunga jua kuna tatizo (menace reflex) na
pia kwa kutumia mwanga wa tochi kumulikia kwa jicho na jaribu kuchunguza pupil kama itapungua na kuwa ndogo then jua hakuna tatizo but kama isipoonesha mabadiliko yoyote jua ya kuwa kuna tatizo mgonjwa anaweza kuwa na mtoto wa jicho (pupillary light reflexes test)....
Jinsi ya kuondoa tatizo ni
kufanyiwa operation (Extra-capsular lens extraction ) na pia kwa kutibu magonjwa nyemelezi ya jicho.....
Hitimisho
- Kula mlo kamili ambao una vitamin A na protein za kutosha
- zingatia usafi wako binafsi na wa mazingira yanakuzunguka
- Na ukijaribu kutumia dawa kwa ajili ya kutatua matatizo yako ya macho sharti uwe chini ya mtaalamu
- Kwa condition yako hapo juu nakushauri nenda kwa hospitali ya rufaa kwa uchunguzi zaidi
- usije jaribu kutumia dawa za miti shamba kuweka katika jicho lako
Kila la kheri kuhusiana na presha ya jicho nishaeleza kwenye post fulani humu ndani jaribu kuitafuta....