Msaada wa dawa za presha ya jicho na mtoto wa jicho

mdauB

Member
Joined
Nov 14, 2017
Posts
5
Reaction score
1
Habari wadau, mimi ni member mpya wa jamii forums. Naomba msaada wa dawa zinazotibu;

Presha ya Jicho
1. Je dawa gani ni nzuri
2. Mtumiaji anatumia kwa muda gani?
3. Matokeo yana anza kuonekana baada ya muda gani?

Mtoto wa jicho
1. Je dawa gani ni nzuri
2. Mtumiaji anatumia kwa muda gani?
3. Matokeo yana anza kuonekana baada ya muda gani?


Natanguliza shukrani.
 
Pole kwa matatizo hayo ya macho yanayokusumbua.....

Hivyo bhasi kwanza tufahamu nini maana ya mtoto wa jicho; Hii ni condition ambayo mara nyingi hushambulia lens ya jicho na hivyo hupelekea kutengeneza ukungu (cloudiness) katika lens ya jicho na hivyo kwa hapo baadae ikishindikana kurekebishwa yaweza sababisha upofu.....

Mara nyingi condition hii huathiri au kushambulia cell mbalimbali za lens na hivyo kuzifanya kupoteza maji, kusinyaa na hivyo kupandiana na hivyo kutengeneza ukungu fulani katikati ya lens hivyo jicho kushindwa kuakisi mwanga vilivyo na hivyo hupelekea mtu ambaye ana ugonjwa huu kushindwa kuona vitu vizuri.....

Vifuatavyo vyaweza sababisha mtoto wa jicho; Yaweza kuwa ya kurithiwa, Yaweza kumtokea mtu mwenye kisukari, upungufu wa calcium (Hypocalcium), kuwa na lishe mbovu, Kuharibiwa kwa layer ya katikati ambayo hutenganisha retina ya jicho na sclera hizo ni baadhi tu....

Upimaji wa macho ili kuweza kubaini tatizo ni kwa kutumia kifaa kinachoitwa ophalmoscopy kujua response ya jicho kwa mwanga na pia kulichunguza jicho kwa ukaribu kubaini kama lina tatizo kwa kujaribu kama kuligusa na lisipojaribu kufunga jua kuna tatizo (menace reflex) na pia kwa kutumia mwanga wa tochi kumulikia kwa jicho na jaribu kuchunguza pupil kama itapungua na kuwa ndogo then jua hakuna tatizo but kama isipoonesha mabadiliko yoyote jua ya kuwa kuna tatizo mgonjwa anaweza kuwa na mtoto wa jicho (pupillary light reflexes test)....

Jinsi ya kuondoa tatizo ni kufanyiwa operation (Extra-capsular lens extraction ) na pia kwa kutibu magonjwa nyemelezi ya jicho.....

Hitimisho
  • Kula mlo kamili ambao una vitamin A na protein za kutosha
  • zingatia usafi wako binafsi na wa mazingira yanakuzunguka
  • Na ukijaribu kutumia dawa kwa ajili ya kutatua matatizo yako ya macho sharti uwe chini ya mtaalamu
  • Kwa condition yako hapo juu nakushauri nenda kwa hospitali ya rufaa kwa uchunguzi zaidi
  • usije jaribu kutumia dawa za miti shamba kuweka katika jicho lako
Kila la kheri kuhusiana na presha ya jicho nishaeleza kwenye post fulani humu ndani jaribu kuitafuta....
 
Ahsante sana,nina kushukuru kwa maelezo yako yaliyojitosheleza, nimejaribu kutafuta thread uliyozungumzia presha ya macho lakini sijafanikiwa kuiona.
 
Kwani kuomba ushauri kwa ID yako ya siku zote ni dhambi?
 
Ahsante nimeona, ninawezaje kuitibu?, nilifanya vipimo nikaambiwa ya kwamba bado uono wangu hauja athiriwa na presha ya jicho
Kama ulienda kupima macho yako halafu wakakuambia hakuna tatizo..... then hakuna haja ya kujitibu mkuu
kwa sababu ishu ya glaucoma iko sensitive sana ndio maana wanashauri mara nyingi uende kwa hospitali za rufaa kwa vipimo na msaada zaidi
 
Kama ulienda kupima macho yako halafu wakakuambia hakuna tatizo..... then hakuna haja ya kujitibu mkuu
kwa sababu ishu ya glaucoma iko sensitive sana ndio maana wanashauri mara nyingi uende kwa hospitali za rufaa kwa vipimo na msaada zaidi
mkuu nilipimwa presha ya macho na nikaambiwa kwamba ipo, then next step ilikuwa nikupima tena iwapo kuna madhara yoyote yaliyoletwa na presha hiyo,baada ya vipimo ikaonekana ya kwamba mpaka sasa presha hiyo haijaleta madhara katika uwezo wangu wa kuona. Nategemea kurudi tena kwa ajili ya vipimo
 
Dawa za Maradhi yote hayo ninazo ukihitaji nitafute kwa wakati wako.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
hivi kwa cataract surgery inaweza gharimu kama kiasi gani kwa makadirio ya chini mkuu??
 
Aksante mkuu kwa ushauri wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…