WanaJF, naomba msaada wenu. Nauliuza hivi -- ule msaada wa USD 700 milioni ulioahidiwa na serikali ya Marekani chini ya mpango wa Millennium Challenge Corp umefikia wapi? Mkataba wa fedha hizi ulitiwa saini wakati aliyekuwa rais wa Marekani Bush alipokuja Tanzania Feb 2008.
Baadaye mwaka huo huo Jk alitangaza kwamba barabara ya Tunduma-Sumbawanga ingeaza kujengwa kwa kiwango cha lami ifikapo december 2008 au Januari 2009 kutokana na fedha za msaada huo. jee hii barabara imeshaanza kujengwa?
Mwenye kujua habari zaidi tunaomba atujuze.