Msaada wa haki na sheria za kazi

Solarpanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2012
Posts
235
Reaction score
38
Habari wote,ni mara ya kwana kuingia jukwaa hili naomba kujuzwa sheria makazini.je sheria inaruhusu mke na mume kukaa ofisi moja,mfano wote mabanker,madoctor nk...na pia je sheria inakataza mke anapokuwa kazini mkoa flani na mume mkoa mwingine tofauti je wanaweza kupewa uhamisho ili wawe pamoja.hapa nina scenario mbili tatu,ya kwanza mmoja alinyimwa uhamisho kumfata mumewe kisa wote watakuwa ofisi moja,na nyingine mwingine alinyimwa uhamisho japo ni ofisi tofaut kisa hakuna sheria inayoruhusu mtu kupewa uhamisho kumfata mumewe,je ni kweli haki hyo haipo tena?asanteni
 
Karibu ktk hili jukwaa mdau, Sio kweli kuwa sheria inakataza mtu kumfuata mwenza, mke anaruhusiwa kumfuata mumewe mara anapohamishwa. Hata pale inapotokea mwanamke anahamishwa mume naye anaruhusiwa kumfuata mkewe katika kituo alichohamishiwa.napia sheria haiwazuii wenza kufanya kazi ktk ofisi. kuhusu hizo sinario naona ni it's just utapeli wa hapa na pale tu.😛arty::humble:
 
Sheria mpya za kazi, ELRA 6/2004, ipo silent. Haitamki kabisa suala la mume na mke isipokuwa tu katika kuzungumzia kifo, au wanapojaliwa mtoto. Katika taasisi binafsi, hili unalozungumza halina nafasi.

Kwa upande wa government, kuna Standing Orders, na kwa kuwa wigo wa taasisi za serikali ni kubwa, kwa uchache hilo suala laweza kupata hekima za kisheria.
 
Asanteni wadau,nw i get the point toka kwenu wote wawili kuwa ni ruksa,sema tu iwe serikalini,poor me wa sekta binafsi na mwenzangu tulionyimwa kisa mimi sheria hairuhusu kumfata na huyo mwenzangu yeye ni cs anaemfata yupo ofic same as yeye.ila dah tuache tu ilivyo
 
kuna sheria zinazotoa au kuelekeza haki za wafanyakazi kwa Tanzania siyo tatizo, tatizo ni usimamizi wa sheria hizo:

Hili swala la wafanyakazi wa ndani si-geni sana kwenye masikio ya wengi, tunayosekta ya wafanyakazi wa huduma za majumbani(Domestic) ambayo kupitia Mwongozo wa Amri ya Kima cha Chini cha Mishahara ya Kisekta Sura ya 300 ya 2010(Regulation of Sectorial Minimum Wage Order Cap 300 of 2010) imeweka wazi kuwa mshahara wa Wafanyakazi wa Ndani(House girl/boy) kuwa ni 65,000/= kwa mwezi kama mfanyakazi atakua anajitegemea kwa kila ikiwemo sehemu ya kuishi, lakini pia atastahili kulipwa pungufu ya 68% kama atakua anaishi kwa mwajiri wake na kumtegemea kwa kila kitu.

Ili Amri hii itekelezwe wapo Maafisa Wakaguzi kwa maswala ya Sheria za kazi ambao wamepewa mamlaka ya kukagua na kubaini ni wapi sheria/amri ya Serikali inakua haitekelezwi ipasavyo, lakini kwa bahati mbaya zoezi hili limekua gumu kutoa matunda mazuri kwani Maafisa hao wanaohusika hawajaandaliwa mazingira mazuri ya kufanya kazi, Serikali inatakiwa ijipange kisawasawa kuhakikisha hawa Maafisa wa wasimamizi wanatekeleza wajibu pasipo mashaka, ili mwisho wa siku Sheria zinazokua zinatungwa zifanye kazi kwa kadri inavyotakiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…