Msaada wa haraka (kisheria) unahitajika.

the event

Member
Joined
Nov 7, 2013
Posts
83
Reaction score
20
Salaam wanajukwaa..

Naomba msaada wenu kisheria wakuu...nitaeleza kwa kifupi kidogo ili nisiwachoshe.

Kuna boss wangu (Indian) aliniajiri yapata mwaka mmoja na miezi saba sasa...lakini wiki iliyopita kwa ghafla tu amenifukuza kazi hali ya kua namdai mshahara wa miezi minne (4) ya nyuma ambayo hakunilipa jumla namdai (3,500,000) biashara tuliyokua tunafanya no biashara ya kuuza simu (smartphones) na sababu kubwa anayotoa ni kwamba kampuni inadai sana watu nje na hao watu wanalipa kidogo kidogo hivyo yeye anataka madeni yake yalipwe papo hapo ambapo ni kinyume na makubaliano yetu tuliyoingia na hao watu tuliowakopesha...sasa ameona kwamba kwakua anadai sana nje (Anadai 10,000,000 tu) na kwamba sisi wafanyakazi (ambao mpka anatufukuza kazi tulikua tumebaki wawili tu wengine wapatao kumi walishaacha kazi mda mref na mishahara yao ambayo walikua wanadai ipatayo ya miezi miwili hawakulipwa mpka leo) tumeshindwa kazi kwasababu kampuni inadai sana nje

"ikumbukwe kwamba wakati tunaingia makubaliano na hao wakopeshwa ni yeye boss aliyetoa go ahead kwaba mali itoke na kwamba sisi tuwe tunakusanya tu paymemt zinazo patikana kisha tunampelekea"

sasa kwakua ameniachisha kazi bila taarifa ya mapema na bila malipo yoyote sasa mimi nimeamua kuliko kuachishwa kazi bila hata senti moja na wakati huo huo namdai mshahara wa miezi minne ni bora niende kisheria zaidi kudai haki yangu.

Lakini tatizo linakuja kwamba kila ninae kutana nae na kumuomba ushauri ananivunja moyo na kuniambia kwamba mahakama haiwezi kunisikiliza kwasababu sina mkataba wa ajira.

"ikumbukwe kwamba tangu tumeanza kazi mimi nikiwa mstari wa mbele pamoja na wafanyakazi wenzangu nimekua nikililia sana atupatie mkataba wa ajira lakini jibu nililokua nalipata ni kwamba (subiri nitawapatia,kama huwezi kusubiri acha kazi) na kwakua hali yangu ya maisha ni ngumu nikaamua kuendelea tu nakazi pasipo mkataba...

Lakini pia sababu nyingine ambayo kwa mtazamo wangu mimi ndiyo iliyomfanya atufukuze kazi na asitupe mkataba wa mda mref ni kwamba..

"yapata miezi wichache iliyopita mimi pamoja na mfanyakazi mwenzangu tulikuja kugundua njia chafu anayotumia kuingiza mali zake hapa dar es salaam pasipo kulipiwa kodi sasa kuna siku alifanya mistake ndogo sana ndipo mimi na work mate wangu tukagundua njia nzima anayotumia" sasa tangu ajue kwamba tunajua ndio figisu figisu zikaanza....

SWALI
1/ Je hakuna kifungu chochote cha sheria kinachonilinda mimi muajiriwa ambae nimeajiriwa kwa miezi nane bila mkataba dhidi ya muajiri wangu?

2/ Je ni kweli mahakama itatupilia mbali maombi yangu kwasababu sina mkata wa kuajiriwa?

3/ Nini cha kufanya ili nipate haki yangu ya mshahara pamoja na fidia ya kuachishwa kazi bila taarifa ya mapema??

Nina maswaliengi sana wakuu lakini naomba mnisaidie kwanza kwa hayo machache kwasababu kesho ndiyo siku niliyopanga kuanza process za kisheria.

NOTE: (Nimeamua kuja jamii forum kwasababu sina uwezo wa kumtafuta mwanasheria nikamlipa) hivyo naombeni msaada wenu kisheria wanajukwaa..

Asante.
===========
UPDATES
===========
Salaam wakuu..

Nashkuru kwa mchango wa kila mmoja wenu..na leo mapema nilifika ofisi za taasisi ya usuluhishi wa mambo ya ajira na nikaambiwa ili nipate fomu ni lazima niende ofisi za TUCTA ili nikapatiwe fomu namba moja...na nikawauliza kwamba " je hata kama sio mwananchama wa tucta nnaweza nikasaidiwa?" wakanambia "ndio" hivyo nikaenda ofisi ya TUCTA na nashkuru nikapatiwa fomu nikatoa kopi 3 na zote nikazijaza maelezo yanayofanana na nikaambiwa niirudishe fomu hyo taasisi ya usuluhishi na nikarudisha fomu hiyo na kwakua tuko wafanyakazi wawili wenye case moja inayofanana hivyo badala ya kuwa na copy 3 kila mtu tulishauriwa tunaweza kutumia hzo hzo 3 kujaza malalamiko ya watu wawili lakini lazima tuambatanishe na barua ya kujulisha taasisi kua ni case ya watu wawili wenye shitaka moja..

baada ya kufanya yote sawia kabisa nikaambiwa fomu zote niende nazo kwa muajiri azitie sign zote kisha moja nimiachoe abaki nayo na mbili nizirudishe kwenye taasisi ya usuluhishi..

KIKWAZO

Kikwazo kikaja kwamba nilipofika kwa muajiri kwakweli sikupenda maneno yake ya utetezi ambayo kwangu mimi naona yalijaa huruma na vitisho kidogo na hofu kwa mbali...hivyo nilipompatia mda wa kuzisoma nakala hizo alimaliza kuzisoma na kisha akaanza kunipaaelezo yake ya utetezi (NIME YA RECORD YOTE) na ilipofika mda wa kusign ili nirudishe aliniambia kwamba hawezi kusign mpka lawyer wake a sign hivyo kama naweza nimiachie zote au nisubiri atanipogia simu..nilipo jaribu kumshawishi ili a sign alikataa na hivyo kunilazimu kumuachia nakala moja iliwanasheria wake aisome na hivyo akimaliza atanipigia nikapewe sign japo najua fika ni mbinu ya kunichelewesha kwakua nafahamu kwamba lawyer hana na huo ndio ukweli fika wakuu japo mnaweza mkaniuliza nimejuaje..ila nimempatia mda aipitie yeye na kama ana lawyer wake na yeye aipitie...
 
Salaam wakuu...najua hili silo jukwaa husika la sheria lakini nimelazimika kupita hapa kwasababu ninahitaji msaada wa haraka kisheria.

Naomba kufahamu je sheria inamlindaje muajiriwa wa kampuni binafsi tu ambae ameajiriwa yapata mwaka mmoja na miezi 7

tafadhali pitia hapa kwa maelezo mapana zaidi☞ https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1132792/

Msaada na ushauri wako ni muhimu.
 
Tafuta mwanasheria akusaidie

Huku utasubiri sana

Na wakija watakwambia uwaone PM
 
Usihofie kuhusu kutokuwa na mkataba maana Zipo test nyingi ambazo Tume ya Usuluhishi na Kazi huzitumia ili kudhibitisha kama mlalamikaji alikuwa mwajiriwa au la! Unachotakiwa kufanya ni kuwahi Tume ya Usuluhishi na Kazi kabla ya siku 30 kuisha tangu ulipofukuzwa, ukifika pale masijala watakupa form no. 1 uijaze kwa utaratibu uliolekezwa/utakaoelekezwa na afisa masijala, ukishajaza, unaipeleka kwa mlalamikiwa ili asaini kuwa amepokea, baada ya hapo unarudisha copy moja kwa Tume ili upewe wito/summons ya kumpelekea mlalamikiwa(summons hiyo itakuwa na trh ya kutajwa/kusikilizwa kesi). Hatahivyo hatuna uhakika kama mlalamikiwa atakataa kuwa wewe haukuwa mwajiri wake ( lakini je kwenye barua ya kufukuzwa kazi amekutambulisha kama nani?) maana akikataa lazima uithibitishie Tume pasipo kubaki shaka lolote kuwa wewe ulikuwa mwajiriwa wa mlalamikiwa ila kama atakubali bhasi wewe utakazia kuthibitisha madai yako ili akulipe. Malalamiko yako yapeleke Tume ya Usuluhishi na Kazi na siyo mahakamani. Je Malipo ya mishahara ya miezi ya awali alikuwa akikulipa kwa cheque, bank deposit au cash?
 
Tafuta mwanasheria akusaidie

Huku utasubiri sana

Na wakija watakwambia uwaone PM
asanye kwa ushauri kiongozi wangu...

tatizo linakuja mwanasheria pesa ya kumlipa sina kwasasa kwasababu nimeachishwa kazi katika mazingira ya mitego sana...yani bos wangu alijua kabosa kwamba kwa kipindi hiki sina akiba hivyo hata akinifukuza sitaweza kichkua mwanasheria wa kunisaidia...lakini na mimi sitaki kukata tamaa na ndio maana nikaja humu...naamini ntapata wasamalia wema
 
Usihofie kuhusu kutokuwa na mkataba maana Zipo test nyingi ambazo Tume ya Usuluhishi na Kazi huzitumia ili kudhibitisha kama mlalamikaji alikuwa mwajiriwa au la! Unachotakiwa kufanya ni kuwahi Tume ya Usuluhishi na Kazi kabla ya siku 30 kuisha tangu ulipofukuzwa, ukifika pale masijala watakupa form no. 1 uijaze kwa utaratibu uliolekezwa/utakaoelekezwa na afisa masijala, ukishajaza, unaipeleka kwa mlalamikiwa ili asaini kuwa amepokea, baada ya hapo unarudisha copy moja kwa Tume ili upewe wito/summons ya kumpelekea mlalamikiwa(summons hiyo itakuwa na trh ya kutajwa/kusikilizwa kesi). Hatahivyo hatuna uhakika kama mlalamikiwa atakataa kuwa wewe haukuwa mwajiri wake ( lakini je kwenye barua ya kufukuzwa kazi amekutambulisha kama nani?) maana akikataa lazima uithibitishie Tume pasipo kubaki shaka lolote kuwa wewe ulikuwa mwajiriwa wa mlalamikiwa ila kama atakubali bhasi wewe utakazia kuthibitisha madai yako ili akulipe. Malalamiko yako yapeleke Tume ya Usuluhishi na Kazi na siyo mahakamani. Je Malipo ya mishahara ya miezi ya awali alikuwa akikulipa kwa cheque, bank deposit au cash?
Asante sana mkuu.

kwanza kabisa malipo alikua ananilipa kwa cash naamini alifanya hivi makisudi ili kuto kuacha alama yoyote ya ushahidi nyuma...

Na pia kuhusu barua ya kuachishwa kazi,wala hajanikabidhi barua yoyote ile mkuu...nilifika tu ofisi asubuh na mapema kuwahi majukumu na nikapokea simu akisema tumeshindwa kazi hivyo tuache mara moja na nilipo uliza kuhusu malipo aliniambia tu kwamba malipo na madeni yako nitakupigia simu uje uchukue,lakini msemo huo ameshawahi kusema kwa wafanyakazi wote wa mwanzo na mpka hivi sasa hakuna hata mmoja aloyewahi kupatiwa mshahara wake.

Na kuhusu kunitambua mimi kama muhusika wake..upo ushahidi wa baadhi ya mikataba ya wateja wetu ambayo mimi niliisimamia na ina majina yangu na pia upo ushahidi pia jumbe zake au sms akinipa majukumu mbali mbali ya kiofisi na pia upo ushahidi wa wafanyakazi wote waliowahi kufanya kazi lwenye hii kampuni wako tayari kutoa ushahidi wao...lakini pia upo ushahidi wa hao wadaiwa ambao tunawadai kwasababu mpka hivi sasa tunapongea wamestop kulipa madeni kwakua mkataba wa kulipa ulikua ni kwamba pesa lazima wafikishe kwangu kwanza sasa kwa sasa walipopigiwa simu na huyo bos kwamba wapeleke pesa walisema kwamba pesa watanikabidhi mimi kwasababu ile document ya makabidhiano inaeleza kwamba mimi ndiye mkabidhiwaji wa paymemt zote

sasa niambie mkuu ushahidi huu nilionao hautoshi kuithibitishia tume ya usuluhishi wa ajira?
 
Ilinikuta hii hadi hii sina hamu nayo mtu unapiga kazi afu jion mtu anasema kazi hauna unauliza sababu nn wala hasemi so hata taarifa before one week sikupewa nilishtukizwa tuu...wachina bhana...nilijawa na presha plus hasira nilishindwa vumilia hata wao pia nilichofanyia hawatasau coz walinipa steress na mawazo bila sababu
 
ulichkua uamuzi gani mkuu?
 
Asante sana mkuu.

kwanza kabisa malipo alikua ananilipa kwa cash naamini alifanya hivi makisudi ili kuto kuacha alama yoyote ya ushahidi nyuma...

Na pia kuhusu barua ya kuachishwa kazi,wala hajanikabidhi barua yoyote ile mkuu...nilifika tu ofisi asubuh na mapema kuwahi majukumu na nikapokea simu akisema tumeshindwa kazi hivyo tuache mara moja na nilipo uliza kuhusu malipo aliniambia tu kwamba malipo na madeni yako nitakupigia simu uje uchukue,lakini msemo huo ameshawahi kusema kwa wafanyakazi wote wa mwanzo na mpka hivi sasa hakuna hata mmoja aloyewahi kupatiwa mshahara wake.

Na kuhusu kunitambua mimi kama muhusika wake..upo ushahidi wa baadhi ya mikataba ya wateja wetu ambayo mimi niliisimamia na ina majina yangu na pia upo ushahidi pia jumbe zake au sms akinipa majukumu mbali mbali ya kiofisi na pia upo ushahidi wa wafanyakazi wote waliowahi kufanya kazi lwenye hii kampuni wako tayari kutoa ushahidi wao...lakini pia upo ushahidi wa hao wadaiwa ambao tunawadai kwasababu mpka hivi sasa tunapongea wamestop kulipa madeni kwakua mkataba wa kulipa ulikua ni kwamba pesa lazima wafikishe kwangu kwanza sasa kwa sasa walipopigiwa simu na huyo bos kwamba wapeleke pesa walisema kwamba pesa watanikabidhi mimi kwasababu ile document ya makabidhiano inaeleza kwamba mimi ndiye mkabidhiwaji wa paymemt zote

sasa niambie mkuu ushahidi huu nilionao hautoshi kuithibitishia tume ya usuluhishi wa ajira?
ndiyo unatosha, huo mkataba wa ukasanyaji madeni utunze sana maana utakusaidia kuthibitisha mahusiano yako na huyo mwajiri, ushahidi upo, wewe fungua malalamiko haraka, ntazidi kukushauri nini cha kufanya.
 
asante sana kiongozi umenipa mwanga sana nashkuru sana...nitakua nakupa updates kila mara ili unishauri cha kifanya
 
sawa, jitahidi pia kutafiti nakala yoyote unayoona itakusaidia kushinda kesi yako, jitahidi pia kuainisha vyema madai yako ya mshahara kwenye form ya madai utakayopewa kujaza huko kwenye Tume.
 
Umesema huna mkataba wa kazi. Sasa hapo utaanzia wapi kesi ya madai yako? Nenda ofisi za wanasheria uwasikilize wana mtazamo gani. Pia uende kwenye chama cha wafanyakazi nafikiri wewe kwa kuwa ulikuwa katika biashara TUICO ndio watahusika.
 
asante kwa ushauri kiongozi nilifika kwenye ofisi za tume ya usuluhishi wa mambo ya ajira na nikapewa maelekezo kua nianzie ofisi za tucta na nikaenda na ninepewa fomu ya kujaza kisha nikarudisha ofisi za tume na pia nikaambatanisha barua ya madai na kwasasa nimepewa tena fomu nipeleke kwa muajiri ili asaini na nirudi tena tume kwa ajili ya kupewa tarehe ya kusikilizwa kesi so mpka sasa naona "so far so good" wacha nimpelekee muajiri japo nna was was anaweza akagoma kusign.
 
  • Thanks
Reactions: Auz

Kila la Kheri! Haki yako hiyo, akigoma nina imani wana njia ya kumuwajibisha kwa mujibu wa sheria
 
Asante sana mkuu.

kwanza kabisa malipo alikua ananilipa kwa cash naamini alifanya hivi makisudi ili kuto kuacha alama yoyote ya ushahidi nyuma...

Na pia kuhusu barua ya kuachishwa kazi,wala hajanikabidhi barua yoyote ile mkuu...nilifika tu ofisi asubuh na mapema kuwahi majukumu na nikapokea simu akisema tumeshindwa kazi hivyo tuache mara moja na nilipo uliza kuhusu malipo aliniambia tu kwamba malipo na madeni yako nitakupigia simu uje uchukue,lakini msemo huo ameshawahi kusema kwa wafanyakazi wote wa mwanzo na mpka hivi sasa hakuna hata mmoja aloyewahi kupatiwa mshahara wake.

Na kuhusu kunitambua mimi kama muhusika wake..upo ushahidi wa baadhi ya mikataba ya wateja wetu ambayo mimi niliisimamia na ina majina yangu na pia upo ushahidi pia jumbe zake au sms akinipa majukumu mbali mbali ya kiofisi na pia upo ushahidi wa wafanyakazi wote waliowahi kufanya kazi lwenye hii kampuni wako tayari kutoa ushahidi wao...lakini pia upo ushahidi wa hao wadaiwa ambao tunawadai kwasababu mpka hivi sasa tunapongea wamestop kulipa madeni kwakua mkataba wa kulipa ulikua ni kwamba pesa lazima wafikishe kwangu kwanza sasa kwa sasa walipopigiwa simu na huyo bos kwamba wapeleke pesa walisema kwamba pesa watanikabidhi mimi kwasababu ile document ya makabidhiano inaeleza kwamba mimi ndiye mkabidhiwaji wa paymemt zote

sasa niambie mkuu ushahidi huu nilionao hautoshi kuithibitishia tume ya usuluhishi wa ajira?
Kwani weee mlokole!!

chukua hizo za madeni ya watu...ujilipe hata kushtaki kwasababu anajua unamdai!!
 
Lakini pia unaweza kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ofisi za huyo bosi zilipo..huwa wanasaidia sana watu kupata haki zao
 
kiongozi salama.

Nilioanga kufanya hivyo hivyo unavyoshauri lakini siku ile ile ambayo aliniambia kazi basi pia alinipiga mkwara mzito kwamba kuanzia siku ile madeni yote yako chini yake na kwamba nosijihusishe nayo..

na hata hivyo tangu siku hiyo nimekua nikipata simu za wadaiwa wetu wakiuliza kua payment wampatie nani na kwakua bos alishasema nisihusike nayo hata kisheria ingeniletea tabu hivyo nikaamua kuwaambia kwamba wadeal na bos
 
Lakini pia unaweza kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ofisi za huyo bosi zilipo..huwa wanasaidia sana watu kupata haki zao
asante kiongozi ila kwakua nimeshafikia hatua nzuri huku kwenye taasisi ya usuluhishi wa ajira basi wacha nione mwisho wake kisha nikiona kuna mkono wa fitna basi nitaenda kwa mkuu wa wilaya
 
Hapa tutakushauri kisiasa tu. Mtafute Wakili umsimulie na akusaidie
Mkuu nimekupata lakini tatizo linakuja ni kwamba ni hivi majuzi akiba yangi yote nilipeleka kwenye kiwanja changu na nilifanya hivyo kwasababu bos mwenyewe aliniahidi paymemt zangu ningepata mwisho wa mwezi uliopita...hivyo hili tukio la kuachishwa kazi ghafla limeniacha bila akiba yoyote hivyo sina akiba ya kumlipa mwanasheria mkuu...ndio maana nikaomba njia mbadala...naomba sana ushauri wako kiongozi wangu
 
Back
Top Bottom