Mkushi Mbishi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 332
- 549
Yeah sure,sema maalezo ya afya mliyopatiwa ni muhimu sana.Hakuna shida yoyote kama ni amemlisha mara moja.
Alafu kama mtoto amewekwa kwenye dawa za kuzuia maambukizi(ARV) uwezekano wa kupata maambukizi toka kwa mama ni mdogo sana,inaweza karibia asilimia sifuri.
Hata kwa mtoto ambaye hayupo kwenye dawa chance ya kupata maambukizi si kubwa sana,ni chini ya asilimia40.
Cha muhimu zingatia maelekezo ya watoa huduma za afya.
Nimekuelewa asanteHakuna shida yoyote kama ni amemlisha mara moja.
Alafu kama mtoto amewekwa kwenye dawa za kuzuia maambukizi(ARV) uwezekano wa kupata maambukizi toka kwa mama ni mdogo sana,inaweza karibia asilimia sifuri.
Hata kwa mtoto ambaye hayupo kwenye dawa chance ya kupata maambukizi si kubwa sana,ni chini ya asilimia40.
Cha muhimu zingatia maelekezo ya watoa huduma za afya.
ArvHabari zenu Wakuu.
Mwanangu amezaliwa wakati mama yake akiwa na tatizo la upungufu wa kinga mwilini,alipangiwa amnyonyeshe kwa muda wa miezi 6 bila kumpatia maji wala chakula chochote mpaka miezi hiyo 6.
Leo amebakisha wiki 2 kutimiza miezi 6.lakini leo nimemkuta mama yangu anampa maji ya machungwa.(yeye hajui kuhusu hali ya mke wangu na mipango ya kumnusuru mtoto)
Sasa nimepata wasiwasi kwa sababu nampenda mwanangu nimeona nije hapa niulize madaktari mnisaidie nawaomba
1.je kulishwa maji ya machungwa akiwa amebakisha wiki mbili kabla ya kutimiza miez 6 inaweza mletea matatizo yoyote?
Naomba mnisaidie wakuu
Hii ya kumpa uji kuanzia miezi 3 naona ni kwa watoto wa kawaida ila kwa huyu wa mleta post kwasababu ya tatizo huwa wanashauri apewe maziwa tu ya mama pekee kwa miezi 6 kwasababu akipewa vitu kama maji na vinginevyo vinaenda kuchubua ndani ya mdomo akinyonyeshwa tu anapata maambukizi.Mtoto miezi mitatu tu unaanza mpa uji kidogo kidogo ije kua hayo maji
Cha kukushauri nenda hospotal ukamwamjie dokta akushauri kitaalam zaidi