Msaada wa haraka kuhusu uombaji wa vyuo vikuu

Usihofu kwa hilo. Kurudiatu!! Nitarudia kwasababu nina shida na nahitaji msaada . AMA KWELI MWENYE SHIBE HAMJUI MWENYE NJAA.
 
As i already said; MWENYE SHIDA NI KAMA SHIMO LA TAKA!! hope you do understand!
 
Umeonae!!! Hata mimi niliona ila nisemee wapi kwa jinsi nilivyoshambuliwa! mwenye shida mara zote hana usemi kwa wenyenavyo!
 
Bado huna sifa za kujiunga chuo kikuu...nakushauri uende chekechea ukajifunze kusoma na kuandika...kabla hujawaza kujaza fomu za TCU!!!
 
Aiseee mkuu wangu...hizi X instead of S mnazipea kitu nn? Pia @ zina maana gan mkuu? Pia Alaka ndio kitu gan?
Kiukwel umeandika kimlugo mlugo sana hueleweki.
 


Napenda kuchukua fursa hii kuungana na wachangiaji wenzangu kuhusu kukukosoa, waliyoyasema sio mabaya na wala usije ukawatafsiri kuwa wana lengo la kukusimanga,la hasha, ila wangependa kuona unazingatia kanuni za uandishi kama zilivyo, ili uitendee haki nafasi yako ya kielimu (kidato cha sita {6}).

Nirudi sasa katika hoja msingi, TCU wanataratibu zao, na ni vizuri zikafatwa, zikipuuzwa huwa zinaleta matokeo mabaya sana! kwa faida ya wengi acha niorodheshe baadhi tu taratibu zao, nazo ni;

i) Wakiagiza ujaze taaluma tano, basi lazima wataweka agizo la idadi fulani ya maombi ya taaluma katika chuo husika. Mfano, usizidishe maombi ya taaluma mbili au tatu katika chuo kimoja. Kwa ulichoamua wewe ni sawa kabisa, taaluma 2 kwenye chuo kimoja na tatu vyuo vingine, sahihi kabisa.

ii) Zingatia ushindani wa vyuo, ili usilipuuze, kama umefaulu kiwango cha wastani, basi omba taaluma za wastani (kwa maana zisizo na ushindani) hali kadharika na vyuo.

iii) Zingatia sana "cut off point", huwa zina maelekezo makubwa sana katika kuchagua taaluma fulani, ukiweka taaluma zote zenye "cut off point" za juu wakati ufaulu wako ni wa wastani, basi kuna nafasi kubwa ya kukosa kabisa chuo.

iv) Kuna hili swala la taaluma zenye vipaumbele na zisizo na vipaumbele, ukweli ni kwamba hiki kitu cha "vipaumbele" hakipo. Nina mifano mingi kuthibitisha maelezo na msimamo wangu. Kwa mfano, wapo waliokosa mkopo huku wakiwa humo humo kwenye hizo taaluma za "vipaumbele"

Kwa kumalizia tu, na kwa faida ya wengi, napenda kuorodhesha vyuo na madaraja ambayo yanapangwa sana katika vyuo hivyo kupitia TCU na sio PRIVATE (except SAUT);

1. UDSM (div 1.3 - div 2.12)
2. ARU (div 1.3 - div 2.12)
3. MUHAS (div 1.3 - div 2.10)
4. MZUMBE (div 1.3 - div 3.15)
5. SUA (div 1.7 - div 3.15)
........................................

Chini ya hivi vitano (5), vinaanza vyuo visivyo na ushindani, kama vile;

6. UDOM (div 2.12 - div 3.17)
7. SAUT (div 3.15 - div 4.19) etc.

Naamini hapa unaweza kupata picha ya daraja lako na chuo unachoweza kupata, tafadhali sana zingatia hizo alama, nakutakia maandalizi mema ya kuelekea chuo kikuu.
 
CHA KUNISHUGHULISHA KWENU MIMI SIKIONI!! CHA KUNIBABAISHA KWENU WALA SIKIONI! You just wasting your time!!
 
Huo uandishi ndo side effect za facebook,Tutafanyaje tena ndo majanga hayo !!
 
hahahaha watoto wa fb hawa tabu tupu hoja ya mcng namshaur mhucka arejee kwenye guide book ya tcu
 

mie mwaka jana niliapply vyuo nane program 1 na ikawa poa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…