Msaada wa haraka kwa mama huyu mjane

Msaada wa haraka kwa mama huyu mjane

Boko halal

Senior Member
Joined
May 14, 2014
Posts
175
Reaction score
124
Kuna mama mjane amenifuata akiniomba nimsaidie kesi yake ambayo amefunguliwa baraza la ardhi la kata.
Kesi yenyewe ipo hivi mme wake ambae ni marehemu kwa sasa (miaka 20 tangu afariki)alikuwa na wanawake wawili yaani yeye na mke mkubwa, mme wake aligawa mali kipindi akiwa hai, ikiwemo mashamba kwa kila mke.
Sasa watoto wa mke mkubwa wanataka mashamba ya mke mdogo, wamefungua shauri baraza la kata, limeanza kusikilikzwa, yule mama amejaribu kujitetea hasa kutumia sheria ile ukomo wa miaka 12 lakini wajumbe wale wamekataa na kuendelea kusikiliza shauri hilo (ni kama mlungula umepita).
Naomba msaada huyu mama afanye ili hii kesi isiendelee kusikilizwa baraza la ardhi la kata ambao tayari wameonesha dalili za upendeleo.
 
Aseme anataka kuweka wakili au aseme shamba lake lina thamani zaidi ya milioni tatu, then itakwenda/itahamishiwa/kufunguliwa mahakama ya wilaya (baraza la ardhi la wilaya).......
 
Aseme anataka kuweka wakili au aseme shamba lake ni zaidi ya milioni tatu, then itakwenda/itahamishiwa/kufunguliwa mahakama ya wilaya (baraza la ardhi la wilaya).......
Hakuna pingamizi la mahakama kwenda baraza la ardhi la kata?
Kuzuia kuendelea na kesi ambayo ipo nje ya ukomo.
 
Hapana, unaweza ukaweka pingamizi la limitation, watahukumu watakavyoona then utakata rufani. Hata hiyo niliyosuggest kama wana hila mbovu na wewe wataendelea na watahukumu, then utairaise kama moja ya sababu za rufaa!
 
Sasa akisema anaweka wakili halafu asiweke itakuwaje maana uwezo wa wakili hana, hilo pingamizi la limitation unaweka kwenye baraza hilo hilo?
 
Ukishakwenda wilayani, hakuna atakayeweka pingamizi kuwa hukuweka wakili. ukiomba rufani, hiyo issue ya limitation utaiibua .
 
Kuna mama mjane amenifuata akiniomba nimsaidie kesi yake ambayo amefunguliwa baraza la ardhi la kata.
Kesi yenyewe ipo hivi mme wake ambae ni marehemu kwa sasa (miaka 20 tangu afariki)alikuwa na wanawake wawili yaani yeye na mke mkubwa, mme wake aligawa mali kipindi akiwa hai, ikiwemo mashamba kwa kila mke.
Sasa watoto wa mke mkubwa wanataka mashamba ya mke mdogo, wamefungua shauri baraza la kata, limeanza kusikilikzwa, yule mama amejaribu kujitetea hasa kutumia sheria ile ukomo wa miaka 12 lakini wajumbe wale wamekataa na kuendelea kusikiliza shauri hilo (ni kama mlungula umepita).
Naomba msaada huyu mama afanye ili hii kesi isiendelee kusikilizwa baraza la ardhi la kata ambao tayari wameonesha dalili za upendeleo.
Mimi ni wakili, nitafute tufanye kazi. Nikionana nae naweza kumsaidia
 
Back
Top Bottom