Msaada wa haraka: Mahindi yangu yana tatizo hili

MLUGURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
2,929
Reaction score
3,710
Leo nimetembelea shambani kwangu nimekuta baadhi ya miche ya mahindi ina hali hii,kwa wataalam naombeni mnijuze hali hii ya kutoboka majani inasababishwa na nini na nichukue hatua gani za haraka
kuokoa mahindi yangu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui ukosefu wa sulphur cjui madini gani nshasahau ila kuna mbolea flani unatakiwa uweke hapo, wajuvi watakuja kukupa majibu kamili na ya uhakika.

By the way mkuu leo umeenda shamba na hakujakucha mkuu, naomba kuuliza ni salama!? misukule hii!!. teh teh!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mkuu, hao ni wadudu ( stalk borer) wanashambulia sehem ya jani changa na mwisho kusababisha Mme a kudumaa na hatimaye kufa. Wahi mapema kwa moja kati ya viuadudu hivi ; duduall au dudumectin au Imida au Atakan au Multi Alpha au Dume au fiprofarm au spidex....ukikosa hizo muombe muuzaji akupe aliyonayo yenye uwezo Wa kuua viwavi
 
Kinachonishangaza na hao wadudu kuacha nyasi na Majani yote yale polininna kuvamia mashamba yetu, mie Miche yangu ya minyanya wameishambukia kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Inatatiza SANA...yaani hawashambulii magugu wala mapori, na msimu wa kilimo ukiisha wanapotea...

Hizi siyo mbinu za kivita za mabeberu kweli??
kilimo kimekuwa cha gharama sana...

Everyday is Saturday...................... 😎
 
pole . chukua kati ya hizi . Piga strong cc 40/16ltr kisha leta majibu hapa

 
Hawo ni wadudu chakufanya tafuta dawa ya kuwauwa sio ugonjwa huo. Ushauri tuu pia unaweza kuchanganya buster humor humo kwenye sumu ya kuuwa wadudu. Tafuta sumu aina ya Multi _Alfa plus, liberate, au spidex

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…