Msaada wa haraka, mtoto kabwia chupa iliyosagwa

Nyabhakangala

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
841
Reaction score
793
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Niende moja kwa moja bila kupoteza muda,

Ni wiki sasa imepita toka niondoke nyumbani baada ya kurudi toka kwenye mihangaiko yangu, nimekutana na taarifa ambazo sio nzuri kuna mtoto wa miaka 9 ambae nilikuwa naishi naye nyumbani kwangu alikuwa anacheza na wenzake.

Kama michezo ya kitoto mnavoijua wakawa wanajipikilisha kama watoto wenzie wanavodai so akawa amemeza unga wa chupa iliyokuwa imesagwa lakini yeye akakaa kimya hakumwambia hata mama yake kwasababu mama yake pia ni mtu wa mishemishe hakai nyumbani, sasa nimerudi ndo watoto wenzie wananiambia hizi habari.

Sasa wakuu naomba kujua;
1-Huduma ya kwanza kwa mtu wa dizaini hii ni ipi?
2-Chupa ikiingia mwilini inachukua muda gani ilikuleta madhara
3-Inaleta madhara gani mwilini.

Naomba kufahamu kwa sasa nipo kwenye usafiri naenda hospitali ili nione kama nitapata msaada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha haaa mi nacheka tu. We mjamaa una akili kweli? Ulitakiwa uanzishe mada baada ya kutoka hosp. Kwa hiyo umekaa hapo kusubiri ushauri kutoka jf? Nonsense..na huo mwandiko usirudie tena!
 
Ila mambo mengine bhana mtu kameza chupa badala ya kukimbilia hospitali we unakimbilia jamii forum sasa mpaka upokee maoni si tayari ashakufa!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi ungeshatangaza msiba hajameza vyupa huyoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu muda wa kupost kusubiri msaada humu unatoa wapi ndugu yangu? mi nlidhan umeshaenda hosp mpaka muda huu umekaa kusubiri kusoma maoni na ushauri? huyo mtoto ni wa nani? c'mon brother sidhan kama muda wa kufikiria hapo ulikuwepo lilikuwa ni suala la haraka kwenda hosp halaf ukatuambia mkasa uliokukuta na pengine kuomba ushauri next time itokeapo. please mpeleke hosp haman haja ya kusbiri kujua madhara yanaanza kutokea baada ya muda gani. kwa kupata tu uhakika lifanyike hilo mapema. ungewah basi muda huu mchukue huyo mtoto uwahi hosp ukirudi nifahamishe please.

 
Chupa nayo ni madini kama ilivokua chuma,calsium na vingine,cha msingi utupe taarifa punde utapofika muda wa kuandika KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA

bichwa baya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…