Pole mpeleke haraka hospitali akapate vipimo ijulikane wazi kwanza anaumwa nini ndipo urudi hapa haraka. Nitajie uzito wake, urefu wake na jinsia yake.
Okay, mpeleke hospitali kwa vipimo. Lakini kwa sasa wakati akijiandaa kwenda hospitali mwambie asinywe chai ya rangi, kahawa, soda yeyote, kilevi chochote, asivute chochote na asile chakula kigumu kinachohitaji maji mengi ili kumeng'enywa na umpe maji glasi 1 kila baada ya masaa 2. Akishapima urudi.asante kwa ushauri.ana uzito wa kg 60, ni mwanamke na ni mfupi sina uhakika ni sm ngp bt ni mfupi
Okay, mpeleke hospitali kwa vipimo. Lakini kwa sasa wakati akijiandaa kwenda hospitali mwambie asinywe chai ya rangi, kahawa, soda yeyote, kilevi chochote, asivute chochote na asile chakula kigumu kinachohitaji maji mengi ili kumeng'enywa na umpe maji glasi 1 kila baada ya masaa 2. Akishapima urudi.
asante kiongozi.umesema akipima nirudi hapa au wapi.
ID yako tu inatosha kukuelezea wewe ni mtu wa namna gani! Unaomba msaada hapa JF kwa mtu mgonjwa kweli? Hivi uko serious kweli wewe? Hujui hospitali zilipo? Muda wa ku-post hapa unautoa wapi badala ya kumuwahisha mgonjwa hospitali? Wiki sasa imepita, wewe leo ndio unaomba msaada! Ama kweli wewe ni Rais wa Migomo, umegoma kumpeleka mgonjwa hospitali badala yake umekubali kung'ang'ana na keyboard ili uombe ushauri JF. Ungekuwa umeshampeleka mgonjwa hospitali kwanza, akapimwa na kupewa ushauri wa kitaalam, mkatimiza maelekezo ya daktari kwa ufasaha lakini bila mabadiliko ya hali ya mgonjwa hapo ungekuwa wa maana sana kuja kuomba ushauri hapa. Ila wewe umeuguliwa kwa wiki nzima, ukakaa kimya (as if you are in comma) ila ulipozinduka ukaja ku-post uzi hapa jukwaani! What a nonsense!salaam wana jf.
naombeni msaada wa haraka.
kuna ndugu yangu anakusa pumzi,unakuta anaanza kukoroma kama mtu aliebanwa koo, then analegea mwili wake baada ya muda unamuona anakakamaa anajinyosha as if mtu anapoteza roho.baadae anapoteza fahamu anakuwa hajitambui.
anakuwa hawezi kupumua hadi umpepee.akizinduka anakuwa nakiu kali kubwa ya maji.ukimuuliza kilichotokea hajui hata kidogo anakushangaa unachomuuliza.
je hili ni tatizo gani???
dawa yake ni nini??? siku zote za maisha yake hajawahi kuwa kuwa na tatizo hili,limeanza kama wiki moja sasa.