Mkuu, inawezekana huyo jamaa anakuchanganya tu, au kweli hiyo pesa haikuingizwa kwenye hiyo akaunti.
Mbaya kuliko ni wewe kutupa pay-in-slip!! too bad, kwenye statement pesa ikionekana haikuingia inakula kwako!
Imeshanitokea NBC, na last week jamaa yangu imemtokea tena. Kuna baadhi ya wafanyakazi si waaminifu. Wanakuchunguza kama hauna tabia ya kuchukua pesa mara kwa mara au kuangalia salio, ukienda au ukituma mtu kuweka hawaingizi kwenye akaunti yako,...wanajikopesha! Nilituma mtu akaenda kuniwekea kiasi cha 5.6M, baada ya siku kadhaa nikaenda kuchukua kiasi flani cha pesa (nikiwa na uhakika kuwa salio langu la zamani ukijumlisha na pesa iliyowekwa inatimia pesa nayohitaji) To my astonishment nikaambiwa salio halitoshelezi!!, kufuatilia hiyo 5M haionekani! Bahati nzuri pay-in-slip iko kwenye file, imegongwa mhuri na sahihi ya teller aliyepokea!!!! Walinipa hiyo pesa na yule jamaa naskia wamemtoa dirishani!!
My take: Tuwe makini sana na pesa, tunza receipt zote za malipo, huo ndy ushahidi wako!