Msaada wa haraka tafadhali kwa kampuni ya kuuza magari ya tradecarview ya Japani

Msaada wa haraka tafadhali kwa kampuni ya kuuza magari ya tradecarview ya Japani

steveachi

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2011
Posts
10,643
Reaction score
12,247
Wakuu habari za mida hii.

Niende moja kwa moja kwenye hoja,kuna jamaa wangu wa karibu sana anataka kuagizia gari Japan kupitia kampuni tajwa hapo juu. Katika kuwasiliana nao wakamtumia invoice isiyo na component ya insurance,yaani badala ya CIF wametumia C&F. Akawauliza endapo meli itadumbukia baharini kwa bahati baya si ndio itakuwa imekula kwake?

Wakamjibu hiyo haina shida na aendelee tu na mchakato wa kuagiza na pia wakamwambia kwamba siku hizi kwa wateja wa Tanzania wanatakiwa wailipie hiyo insurance kupitia kampuni ya Bima ya Tanzania na ikitokea shida yoyote wao ndio watakaocover ajali.

Sasa akaniulizia mimi kuhusu huo ukweli nikawa sijui lolote lile,ndio nikaamua na mimi nililete humu hili suala kwa kuwa penye wengi hapaharibiki jambo. Je ni kweli akiagizia hakuna shida yoyote.

Naombeni majibu tafadhali.

Nawasilisha.
 
Mimi kwa upande wangu nimeshaagiza gari kama mbili kupitia tradecarview kwa malipo ya CF na sijapata shida yoyote.Zile meli ambazo zinasafirisha magari ni nadra sana kupata ajali we mwambie asiwe na wasiwasi anunue tu
 
Thanks mkuu,nashukuru sana kwa kunitia moyo
 
CIF hiyo I ni Insurance kama maelezo kwenye post #2. Ukitaka kulipia Insurance nadhani ni USD70.
 
Back
Top Bottom