Msaada wa haraka tafadhali; Tiba ya matiti kuvimba na kuuuma kunakopelekea homa kali.

Msaada wa haraka tafadhali; Tiba ya matiti kuvimba na kuuuma kunakopelekea homa kali.

Sokulu Mkombe

Senior Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
126
Reaction score
167
Natumaiani hamjambo wana JF

Nina ndugu yangu Umri ni 50+ anasumbuliwa na tatizo la matiti kupata maumivu makali ya kujirudia rudia hasa upande kushoto yanayopelekea uvimbe, na hujihisi joto pindi yanapoanza kuuma.
Maumivu hujirudia baada ya muda (Mf wiki 1 au 2). Ni tatizo la muda mrefu kidogo takriban miaka mitatu kwa mujibu wa mgonjwa.

Historia ya MATIBABU
1.
Ametibiwa (Pima) wilayani Ugonjwa haukuonekana
2. Muda huu nipo nae Hospitali ya Rufaa kanda MBEYA na tumepima vipimo vifuatavyo na havijaonyesha kitu ( Hawaoni ugonjwa)
- Mammography
- Ustasound

Amepewa Dawa (BRUSTAN) na ameambiwa arudi tena kupima baada ya mwaka.

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanye nini?

Najiuliza ataishi vipi ndani ya huo muda ikiwa tatizo bado halijapatiwa ufumbuzi na bado anaumwa.

Natanguliza shukrani
 
Pole ya mgonjwa nakushauri atafute maua ya periwinkle achukue miziz yake kama kias cha robo hivi achemshe awe anatumia kutwa ×3 ndan ya wik 2...3 ajitahidi ayapate hayo mrejesho utaleta

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ndo haya?
 
Attachments

  • IMG-20220826-WA0008.jpg
    IMG-20220826-WA0008.jpg
    97.9 KB · Views: 49
Back
Top Bottom