Msaada wa haraka tafadhari.

MoneyHeist4

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2017
Posts
2,134
Reaction score
3,192
Mpenzi wangu anaujauzito takribani week sasa, lakini tumbo linakuwa linamuuma sana pamoja na kuchoma choma na ni mimba yake ya kwanza.

Shida ni nini? Maana sielewi kabsa anavyolalamika tumbo linamchoma mno muda mwingine nashikwa na hofu kwamba mimba inaweza kutoka. Maana aliwahi kunambia ana tatizo la chango(mchango).

Kama kuna tiba tafathari nisaidieni. [emoji25][emoji25]
 
Epuka sana kumlisha mkeo kande. unaona sasa madhara yake
 
Moja kati ya dalili za hatari (danger sign) kwa mama mjamzito ni maumivu makali ya tumbo. Usikae nae hom muwahishe hospitali
 
Maumivu ya tumbo huwa kawaida wakati wa Ujauzito unaweza kuwa mara nyingi huwa ni Cramping(kutanuka kwa uterus na Ligaments Pia) Ila pia Inaweza kuwa hatari na kupelekea Miscarriage..Mpeleke Hospitali Mkuu!
 
Hivi wanajamii mbona wagumu hivi huelewa, mtu anaumwa unakimbilia humu kuomba ushauri badala ya kumpeleka hospital, hebu tubadilike kwanza tuwapeleke wagonjwa hospital ikishindikana ndio tuje tuombe ushauri. Mwenyezi mungu amfanyie wepesi apone haraha mgonjwa wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…