Msaada wa haraka unahitajika enyi ndugu, tafadhari pita hapa

Je ulifanya hicho kipimo cha tezi dume kama ulivyoshauriwa?? Majibu ya kipimo yalikuwaje??

Kuhusu hospital gani uende, unaweza kwenda Muhimbili , Regency, Hindumandal au Kairuki hospital kwani hospital hizo zote zinakubali bima ya afya NHIF na wana Urologists,

Nakushauri wahi upesi hospital ukaonane na Daktari bingwa, tatizo lako unaonana na madaktari general ambao wanaishia kukupima urinalysis tu na kukupa dawa za UTI.

chelewachelewa utamkuta mwana si wako ndugu!!
 
pole sana mkuu nenda hospital kubwa angalau upime ujue tatizo nn.kujua tatizo ni moja ya tiba pia
 
Mkuu moghasa labda wakati wa kutafuta tiba ulikopita huko na huko wataalam walikwambia chanzo cha tatizo lako ni nini?
Wengi walihis ni tezi dume BT kwa umri Wangu dkt akasema
Sasa mkuu labda niulize hapo walipokushauri upime tezi dume je ulipima maana hili haukulitolea mrejesho..
Nilipima mkuu wakadai iko normal pia kwa umri Wangu 28yrs kama haiwezekani kunipata !
 
Jaribu Lancet Lab jengo la Doctor's Plaza pale Morocco mita chache kutoka jengo la Airtel..wana vipimo vya kisasa vya aina nyingi so itakuwa rahisi..na NHiF wanapokea..Polee sana mkuu..
 
izo zingine huwa ni kama adhabu vipi haukuchepuka na mali ya mtu lakini maana kama wataalam wanasema hakuna tatizo inabidi ugeukie upande wa pili
ni ushauri tu
 
Ukizunguka kote, wakishindwa njoo tukupe mizizi ya magonjwa ya kiume.
NB. Mizizi ni ya uchungu shubiri haioni ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…