Msaada wa haraka unahitajika :sheria inasemaje juu ya jambo hili?

charrote

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
1,848
Reaction score
4,146
Habari za muda huu.
Nahitaji kujua sheria inasemaje juu ya suala lifuatalo.

Kaka yangu alitengana na mwenza wake miaka miwili iliyopita. Akalazimika kuwachukua watoto watatu aliozaa nae na kuishi nao. Miezi saba baadaye mwanamke akaenda kumshtaki mume kuwa amemtelekeza na ana ujauzito, (wakati anaondoka hakusema ).Mwanaume akaamriwa kutoa matunzo. Wakati fulani mwanamke aliomba pesa ya mtaji ili aendelee na maisha yake akapewa na ikaandikwa kabisa. Baada ya muda akarudi tena kushtaki akiwa na mtoto tayari mwanaume akaamriwa tena kuendelea kutoa matumizi. Sasa mwezi huu mwanaume alikwama kiuchumi na akatoa taarifa lakini mwanamke haelewi na mpaka sasa ameleta barua ya mwanaume kuitwa TAWLA .je sheria inasemaje ikiwa mwanaume atashindwa kutoa pesa hiyo? Kuna uwezekano akapelekwa mahakamani na kufungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…