Msaada wa Haraka unahitajika

Msaada wa Haraka unahitajika

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Posts
3,335
Reaction score
6,186
Kuna rafiki yangu maisha yake yalikua mazuri sana alikua mjasiriamali mzuri amepata hela za kutosha.

kwa bahati mbaya miezi kama 4 nyuma alivamiwa na majambazi wakampora kiasi kikubwa cha hela
alikua anataka kusafiri kwenda njee kununua mzigo.

Wakati anaugulia maumivu ya kuibiwa Duka lake moja likaungua moto 4 weeks ago. sasa kijana wa watu
amechanganyikiwa anahisi kama dunia imemgeuka anataka kuhama mjii akakae kusikojulikana anata kuuza nyumba

Ahamie sehemu ingine probably ataaweza kuanza upya. Kuna mkopo wa 12m anadaiwa bank anahisi bank watakuja kuuza nyumba yake

Nimejitahidi kumshauri imkua ngumu. Nimemuomba niandike habari yake hapa bila kumtaja kwa jina then yeye afuatilie ushauri wenu hapa amekubali hivyo tumsaidiaje?

wenu
 
Pia tumekubaliana kama atapat ushauri wa kumfaa nitaweka number yake ya simu (hana email) ili kama kuna ambaye anataka kushauri moja kwa moja kwenye simu aweze kufanya hivyo
 
pole sana

kwa tanzania hakuna jiji la biashara kama daresalaam

so kuhama ni ujinga

anatakiwa kujifunza namna ya kuhifadhi na kufanya transactions za pesa kwa usalama zaidi

huko atakapokimbilia hakuna majambazi???????/
 
Heeeeee hii ndio mitihani ya maisha pole yake kwanza, mwambie kwenye maisha kuna kupanda na kushuka, na biashara hivohivo, na kama yeye ni mfanyabiashara halisi hatakiwi kukata tamaa, unawaona kina Mengi hawa usidhani huwa hawakwami, ila wanatafuta njia za kuinuka tena, hapa kwa kweli ndio nimekumbuka ile characteristic ya "entrepreneur are born not made.......... au yeye alibahatisha tu kuwa mfanyabiashara....... mwambie biashara zoooote zina matatizo, atafute tu namna ingine ya kuanza from the scratch
 
Mh hiyo story ya kweli? Na hizo hela alizochukua benk dhamana yake ni nini? Toka alivyochukua amerejesha mara ngapi?
Au anataka kufunga kipindi benk? Awe wuwazi asaidiwe m12 anataka kukimbia jiji na bado ana nyumba dar? SIJAELEWA .
 
Heeeeee hii ndio mitihani ya maisha pole yake kwanza, mwambie kwenye maisha kuna kupanda na kushuka, na biashara hivohivo, na kama yeye ni mfanyabiashara halisi hatakiwi kukata tamaa, unawaona kina Mengi hawa usidhani huwa hawakwami, ila wanatafuta njia za kuinuka tena, hapa kwa kweli ndio nimekumbuka ile characteristic ya "entrepreneur are born not made.......... au yeye alibahatisha tu kuwa mfanyabiashara....... mwambie biashara zoooote zina matatizo, atafute tu namna ingine ya kuanza from the scratch
hapo pamenigusa, na ili uwe entrepreneur halisi lazima uwe risky taker, is he willing to risk , na enyi wafanyabiashara wengine mjifunze unasafiri kwenda nje kibiashara, mahela unakaa nayo ya nini? hivi travellers cheque siku hizi hazifanyi kazi?mwambie aanze upya mwanaume hakimbii shida huwa anaikabiliana nayo
 
Mwambie ani PM details zake, tulitaftie ufumbuzi...je anamaadui? Alishadhurumu?
 
Kamwambie kwamba kinyuma cha faida ni hasara...Kwa hiyo wakati wowote alipokuwa anachekelea kwa kutembelewa na faida..hasara na ndugu zake walikuwa wamenuna...Akikubali hilo atakuwa amepiga hatua kwenda mbele!!

Mweleze kwamba ana bahati kubwa kwa sababu tayari ana nyumba..Hatafukuzwa na mwenye nyumba..Aende bank wajadiliane jinsi ya kumpa mkopo mwingine ili asife kabisa kibiashara..Hiyo ndiyo kazi yao...kuhandle wanaochekelea na wanaolia pia!!
 
Tena siku hizi unalazimishiwa mkopo kabisa
 
Tena siku hizi unalazimishiwa mkopo kabisa

Lazima Bank itakuwa tayari kumsikiliza na kumpatia stimulus package...sisi wengine wajasiriamali lakini mikopo ya kuongezea nyumba ndogo tunachukua kila mara. Watashindwaje kumsikiliza mteja wao? Bank haina shida ya kuuza nyumba labda kama wamefikia mahali ambapo wanalazimika kuokoa pesa zao!!

Ngona niwasiliane na Ex-GF wangu ambaye ni afisa mikopo wa bank fulani nisikie anasemaje!!
 
Ngumu kumeza, mkopo wa m 12 anakimbia mji wake? ajikaze kiume aanze upya
 
Atauzaje nyumba kwa kuogopa Bank wataiuza?kwani alipokopa bank dhamana ilikua ni nyumba?if yes ataiuza vp sasa na hati ipo bank?

Kama alipokopa nyumba haikua dhamana sasa mchecheto wa nn?kawaida bank wanauza ile dhamana uliyoweka na hati wanakua nayo wao.
Mwambie atulie apige kazi pesa ipo tu haina mwenyewe cha muhimu kusugua kichwa tu.
 
Mazingira ya hizo issues yanahitajika ..Kuna maswali kama

Je? anajiona maisha yake yako hatarini hasa kuhusiana na deal alizokuwa anafanya?

Inaendana na swali la hapo juu..Je? Biashara aliyokuwa anafanya ilikuwa ni halali au ile ya kimjini mjini au misheni town..ambayo sometimes jamaa wanapata kishawishi cha kudhulumiana na kulipizana kisasi..

Je? ana rasilimali (investments) zaidi ya hiyo biashara aliyokuwa anategemea. Hapa anaweza kuchepuka na kuhamishia nguvu na kuendelea na upande wa pili wakati anajijenga upya.

Kwa nini anaogopa bank.. alipata mkopo kihalali au kimjini mjini...na alikuwa halipi na anawasumbua watu wa bank?

Mwisho mwambie kama alikuwa anafanya mambo halali mjasilimali (entrepreneur) hakati tamaa na pia ni risk taker mkubwa..matukio yatamsaidia kumfundisha kuwa makini sio tu katika biashara ila hata maisha ya mtaani..ili akiwa na ka pesa kidogo asiwe anatamba sana vijiweni na kujichora..
 
"running the problem is not solution to the problem" Akae chini ajipange upya. Ndo mitihani ya maisha hio.
 
Back
Top Bottom