Msaada wa Haraka wa Kisheria nimesimamishwa Kazi Kesi J3

Mwinjilist mtume nabii

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2015
Posts
2,437
Reaction score
1,097
Kuna mfanyakazi wa Kampuni ya Sukari Kilombero alisimamishwa kazi,,,,,kwa madai eti alipost taarifa ya kampuni kwny mtandao bila kibali.

Ni kwamba kulikuwa na mvutano Wa nyongeza ya mshahara kati ya mwajiri na chama cha wafanyakazi ambapo w/Kazi walichagua kutaka kugoma, na Katibu mkuu Wa TPAWU Taifa Mh Kabwengwe akatoa waraka Wa kuruhu mgomo huo. Lakn kabla ya cku ya mgomo kufika ,, Kampuni ikatoa nayo waraka Wa kupinga mgomo huo kwa kusema haukufuata sheria


Sasa waraka huo wa Kampuni ndio mfanyakazi huyu aliuweka kwenye facebook ili kuwajulisha,,,,,,ndipo hapo uongozi Wa Kampuni unasema amefanya makosa kutuma kwny mtandao.
SWALI

1. Je hilo ni kosa???

2. Kesi no J3 kaambiwa aende na mashaidi,,,je mashaidi ni lazima wawe nao ni wafanyakazi was kampuni hii????? Au MTU unaemwamini???

3. Naomba kujua na vifungu vya utetezi hapo
 
MKATABA WA AJIRA Yako na co. policy yenu zinasemaje juu ya issue iyo
 
Mchungaji si umfanyie maombi tu kwani kuna sababu ya kutafuta msaada wa kibinadamu?
 
Mkataba unasemajee?
Yeye aluvyopost kwenye mitandao kwani ndiye afisa habari wa kampuni??
 
Mikataba mingi ina policy kuhusu media.Moja ya makatazo ni hilo la kuongelea issue yeyote inayohusu kampuni kwenye media.

Msemaji wa kampuni ndio mwenye mamlaka ya kusema kwenye media kwa niaba ya kampuni.
 
kafanya kosa, maana huwa kuna msemaji wa kampuni, kwanini yeye alipeleka kwenye social network ili hali si msemaji?

Pia lazima ujue kila kitu kina taratibu zake sijui yeye kabla hajaweka fb alifuata taratibu zipi kwa walio juu yake, ila lazima ajue hapo pia atashukiwa kwakuhamasisha mgomo mahali pa kazi. Ngoja waje wataalamu watakusaidia.
 
Yeye alipost lile tangazo baada ya uongozi wa kampuni kuwa umeshalitoa tangazo hilo,,,,,ndipo akalipiga picha na kuliweka kwny fb akiwajulisha wafanyakazi kuwa mgomo umesitishwa. Ndo hapo kosa wanasema
 
Yeye alipost tangazo la kampuni lililositisha kufanyika kwa mgomo akiwajulisha wafanyakazi,,,,,,,,,,,,kwasbb wengi walijua mgomo utakuepo,,,,sasa wkt tangazo linabandikwa yeye ndio alikua kazini,,kwa iyo waliokua nyumban wasingeweza kujua,,,,na ukizingatia tangazo lilibandikwa kwny Notice board ndani ya kiwanda ambapo huwez kuingia kama haupo zamu.
 
Dah!!! Ngoja wajuvi waje watakusaidia
 
Hivi nyie hamjamuelewa mchungaji apo huyo MTU anaezungumziwa hapa ni yeye mwenyewe na kimbelembele chako cha kuletaga hapa huku habari za huko kilombero sasa utanyooka wewe unajipa kazi za upr sio?
 
Kwanini usiseme muhusika ni wewe mwenyewe?
 
Hivi nyie hamjamuelewa mchungaji apo huyo MTU anaezungumziwa hapa ni yeye mwenyewe na kimbelembele chako cha kuletaga hapa huku habari za huko kilombero sasa utanyooka wewe unajipa kazi za upr sio?
Tumeshaelewa ni yeye mwenyewe ila tumsaidie kwa mawazo maana makosa ni sehemu ya maisha kwa binadamu
 
Nakushauri kama kesi ni J3 kesho waombe wakupe muda uweze kumtafuta mwanasheria akusimamie ili ujipange usije ukapanic ukaharibu. Kisheria wanatakiwa wakupatie muda huo hata kama utakuwa mfupi kiasi gani, then mtafute mwanasheria hata maeneo ya karibu na ww ili uweze kumudu gharama zake, mpe full scenario ya suala lako naamini atakusaidia vizur sana. Otherwise pole sana.
 
Ni kosa ila inategemea mkataba wake ulikuwa unasemaje kuhusu utoaji wa taarifa za ndani za kampuni..

Mfano kampuni nyingi binafsi huweka kifungu kwamba taarifa zozote kuhusu kampuni zinatakiwa zitolewe na Idara husika..

Kama yeye alijifanya afisa habari itakula kwake..

Tuwe makini..


Over...


Ethos
 
Yaan kwenye mikataba yote ya wafanyakazi,,,hawajaweka hicho kipengere kabsa,,,,kuna sheria za kawaida kabsa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…