msaada wa haraka wana jf

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
3,840
Reaction score
659
Wanna jf nina ndugu ameathirika Leo asubuhi amekuja Kwangu nilivyo muona amebadilika ametokwa na upele.
Msaada naoutaka ni sabuni gani na mafuta ambayo anaweza tumia akakausha upele.
 
Mpeleke hospital akaonane na wataalam anaweza pata matibabu na ushauri pia
Kuliko kujichukulia maamuzi binafsi
 
mpeleke hospitali kubwa kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi, kesho ni Jumatatu
 
Wanna jf nina ndugu ameathirika Leo asubuhi amekuja Kwangu nilivyo muona amebadilika ametokwa na upele.
Msaada naoutaka ni sabuni gani na mafuta ambayo anaweza tumia akakausha upele.

Sasa Mkuu kweli hata wazo la kwenda kuonana na daktari halipo?!! Unajua mwili ukiwa na virusi kinga inapungua sana kwa hiyo magonjwa nyemelezi ni rahisi sana kupenya, hospitali ndiyo sehem muafaka ya kupata tiba mkuu, pia kama tayari anatumia dawa inabidi kuhakikisha anazitumia ipasavyo, chakula anakula ipasavyo? pia anahitaji tiba ya nafsi, asikae na mawazo sana, kama hana kazi mumtaftie kitu cha kumweka busy. Siku hizi ukimwi ni ugonjwa wa kawaida sana kama mtu anafuata kanuni bora za afya, binafsi naogopa kisukari kuliko ukimwi.
 
Mpeleke hospitali na afuate masharti ya tiba...msimwogope hadi akajistukia na kujiona maiti inayotembea na hapo mtakuwa mmeshiriki kumwua mapema while siku hizi watu wanaishi na maradhi hayo miaka kibao wanakuja kufa kwa vitu vingine kama ajali n.k
 
Nisaidie hospital gani nzuri naweza kwebda mpeleka
 
Kiongozi ina maana ulishindwa hata kumpatia msaada wowote hadi kuamua kumuanika hapa jamvini? Hudhani huu ni unyanyapaa mambo leo?
 
Kiongozi ina maana ulishindwa hata kumpatia msaada wowote hadi kuamua kumuanika hapa jamvini? Hudhani huu ni unyanyapaa mambo leo?

hajamtaja jina bana, hivyo hajamwanika kwa vyovyote vile, yuko kwenye juhudi ya kumtafutia dawa ndiyo maana kasema wazi tatizo linalomsumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…