Msaada wa jinsi ya kukaanga karanga

Msaada wa jinsi ya kukaanga karanga

The Initiator huru

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
1,993
Reaction score
2,635
Hello, wakuu naomba msaada wa jinsi ya kukaanga karanga kwa ajili ya kuuza. Je, naweza tumia microwave katika kukaangia karanga au je, nitumie nini katika kukaanga karanga?

Msaada tafadhali
 
Angalia video you tube utapata ujuzi zaidi
 
Binafsi karanga huziandaa katika sufuria utia kijiko kimoja cha maji na utia chumvi, pilipilli na Iliki uzigeuza ipasavyo kisha kuweka katika moto kiasi.

Muda wote uhakikisha nageuza. Baada ya muda zikisha kwiva uziondoa na kuziweka katika combo cha wazi (Sahani). Tayari kwa kuliwa

Huandaa zangu za kutafuna maana ni mpenzi mkubwa wa karanga.
 
Dah asante
 
Ebu jaribu hii idea alafu utanipa mrejesho.

Chukua karanga zioshe vizuri kisha zipate jua zikauke, zikishakauka zitoe, chukua sufuria lako tia mchanga wa kujengea/mtoni mix karanga na chumvi mule ndani kaanga huku unageuza kama vile unapepeta mchele kwa kutumia mikono miwili.. hii idea niliiona miaka mingi iliyopita nikiwa bado kinda
 
Sababu ya kuziosha ni ipi kama zinaivia kwenye mchanga?
 
Nafanya hivyo pia lkn sijawahi weka pilipili. Ni pilipili ya unga?
 
Sababu ya kuziosha ni ipi kama zinaivia kwenye mchanga?
Labda kuondoa fangas🙄
Baada ya hapo huwa naziosha na maji yenye chumvi nazikausha juani ili chumvi igandiane na karanga. Then nazikaanga kwa kutumia mchanga.
Baada ya hapo naweka kwenye kikapu naingia mtaani bar, stendi etc kuziuza.
 
Sababu ya kuziosha ni ipi kama zinaivia kwenye mchanga?
Hapo amejichanganya ,unaziloanisha unaziweka chumvi unazianika halafu unachukuwa mchanga usiokuwa na vumbi unaweka kwenye chombo cha kukaangia unaweka jikoni ukipata joto unaweka karanga unakaanga zikiwa tayari unazipembua.
 
Mi mvivu kuandika but ntajitajitahidi,kwanza kabisa changanya maji kiasi na chumvi halafu anika juani,zinapoendkea kukauka washa jiko lako la mkaa,nunua chumvi ile ya 500 kama kwa kg 1 au moja na busy,Kama zaidi ya hapo nunua pakti 2,karanga zikikauka is chumvi katika sufuria kulingana na wingi wa karanga,iache chumvi ipate Moto.Ikishakua ya Moto weka karanga zako endelea kuzigeuza ukiwa umeshika sufuria huku na huku,zitaanza kubadilika rangi kuwa nyekundu pia uliaji wake unabadilika kulingana na jinsi zinavoendelea kuiva ,utaonja utapoona umeridhika unavoonja basi zitakuwa tayari kwa kuuzwa,chumvi acha ipoe itunze utatumia wakati mwingine.NIMEWEZA NADHANI,USIPOELEWA KARIBU UNIULIZE.
 
Ebu jaribu hii idea alafu utanipa mrejesho.

Chukua karanga zioshe vizuri kisha zipate jua zikauke, zikishakauka zitoe, chukua sufuria lako tia mchanga wa kujengea/mtoni mix karanga na chumvi mule ndani kaanga huku unageuza kama vile unapepeta mchele kwa kutumia mikono miwili.. hii idea niliiona miaka mingi iliyopita nikiwa bado kinda
Hizi njia za kizamani hazifai kwa sasa. Waachie wapogoro 🤣
 
Hello, wakuu naomba msaada wa jinsi ya kukaanga karanga kwa ajili ya kuuza. Je, naweza tumia microwave katika kukaangia karanga au je, nitumie nini katika kukaanga karanga?

Msaada tafadhali
Zamani enzi hizo ndugu yangu anauza UJUGU (KARANGA) ,alikuwa anaziosha anaweka chumvi anaanika,
Zikikauka anakaanga mchanga mpaka unapata moto KWA kugeuza geuza kisha anaweka KARANGA anakaangia humo kwenye mchanga,
Inatoka na taste grade A
 
Nunua mashine ya popcorn uwe unakaangia au Air fryer ipo kama Oven.
 
Back
Top Bottom