gumboot
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 263
- 93
Habari zenu,
Niko hapa kuomba ushauri wa kiafya juu ya mtoto wangu mwenye miaka mitatu na nusu,Nimehangaika nae saana ila naona hamna mafanikoio,tatizo kubwa ni upumuaji kama nilivoandika yaani wakati wa usiku hii hali ndo inazidi anabanwa kuanzia puani hadi kwenye mbavu na kutoa sauti ambayo huninyima usingizi siku zote.
Hii hali ni toka azaliwe,alizaliwa kwa operation ila baada ya trial na kupata low score kama walivosema wataalamu .
kapata chanzo zote ila jamani nimeisha mpeleka hospital hadi huruma,maana nilimpepeka m/nyamara mara ya kwanza nikiwa natafuta referal ya muhimbili basi pale alichomwa sindano za kutosha ninayoikumbuka jina ni gentamicine na hapo tulikaa siku tanao nikidhani nitapata referal ila madakitari walisema ni pneumonia ikabidili nikubali ila tu baada ya siku kidogo hiyo hali iliendelea ,nikaenda kwa kwa koya nikapewa dawa za vidonge alipata nafuu kidogo ila baadae hali ilirudi nilivorudi pale dawa zikawa zilezile na hapakuwa na mabadiliko ,watu wakanishauri niende kwa Dr.Amir ,yeye alisema ni pumu alichomwa sindano na kupewa sulbutamol inherer akapata nafuu kidogo baadae hali ilirudia wakati bado anatumia zile dawa.
Nilianza kuona tatizo ni tata ila sikukata tamaa nilimpeleka kwa Dr.Massawe akasema hajaona ugonjwa ila nilihudumiwa na Dr.Dulla basi ikabididi niondoke.Ila kwa sababu mtoto anapumua kwa shida niliendelea na hospitali nyingine ya Dr.Ole pale magomeni baada ya kuelekezwa kwa kuna mtaalamu wa ENT basi hapa alipigwa X-ray na kuona kuwa ananyama puani,basi akafanyiwa operation ya kuondoa nyama hizo,akawa kama amepata nafuu kwa miezi sita,ila baada ya hapo hali imerudia na nimeisha mpeleka sanitas lakini waapi ...
Sasa kweli nimechanganyikiwa kwani afya yake inazolota kutokana na upumuaji mbaya na hospitali zetu jamani wanachukulia mambo kirahisi sana yaani mtu unaeenda hospitali kwa nia kabisa ila huduma si nzuri.
Samahani kwa kuandika kwa urefu ila nina mengi maana naomba msaada wa hospitali nzuri itakayo weza kumsaidia mtoto wangu ,ushauri au tiba mbadala.
Asanteni