Msaada wa kiafya

nsalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
1,189
Reaction score
1,240
Mimi nina tatizo la kisukari. Toka ijumaa najisikia vibaya nasikia kutapika mwili hauna nguvu, natokwa na jasho, kizunguzungu na kuchoka. Nimeenda hospitali nimepima malaria sina, mkojo sina maambukizi na sukari ipo 9. Hii hali inaweza kuwa nini maana inanikosesha raha kabisa.
 
Jibu unalo. Hicho ni kisukari tu. Normal blood glucose inatakiwa iwe isipungue 3.3mmols/dl na isizidi 6.6mmols/dl. Kwako ipo 9mmols/dl hiyo ipo juu sana.
CHA KUFANYA
NENDA HOSPITAL KUBWA HARAKA HIYO SI DALILI NJEMA.
MENGINE UNAYOWEZA KUFANYA NI:-

1. Nunua machine ya kupima blood glucose. Jifunze kuitumia pindi unapojisikia vibaya. Bei zake ni kati ya 50,000 na 100,000 at any pharmacy shop.

2. Badili aina ya vyakula unavyokula acha sukari na jamii zake pia wali na sembe haufai kwako.

3. Tumia dawa inaitwa diabenese kushusha sukari. Kidonge kimoja kila siku asubuhi. Hakikisha unapima sukari isishuke sana.

4. Muone daktari kwa ushauri zaidi
 
Asante ndugu yangu kwa ushauri mzuri huo. Niliuliza kwa sababu sijawahi kujisikia namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…