Msaada wa kilimo cha chikichi(maweze)

Msaada wa kilimo cha chikichi(maweze)

Tangantika

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2018
Posts
5,586
Reaction score
7,087
Naomba mwenye kujua uendeshaji wa kilimo cha chikichi kwa heka moja kuanzia kupanda mpaka kuanza kuvuna kwa mbegu ya miaka 3/4.kiwango cha mafuta unachopata kwa heka kwa mwaka wa tatu, nne na kuendelea.
 
Kilimo Cha Michikichiki Hakina Gharama Mkuu!
Mwaka Wa Kwanza, Kama Unalo Shamba, Tafuta Mtu Umpe Alime Bure, Na Apande Mahindi, Maharage, Karanga, E.t.c! (hapa Kijijini Kwetu, Watu Wanahitaji Sana Maeneo Ya Kulima, Hata Kwa Kukodi, Ila Wenye Mashamba Hawayatoi, Ubinafsi Tu). Hivyo Basi, Ukimpa Mtu Alime Shamba Lako, Kwanza Umepunguza Gharama Za Kuliandaa Shamba Lako.
 
Mwaka Unaofuata, Muda Kama Huu, Tafuta Mtu Aliandae Kwa Ajili Ya Kupanda Mahindi , Mihogo Na Karanga (muhimu Sana Hiyo) Ile Mvua Ya Mwezi Wa 10 - 11 Inaponyesha, Wewe Umeshaweka Miche Yako Shambani. Baada Ya Hapo, Yule Aliyepanda Mahindi Shambani Kwako, Akienda Kupalilia Mahindi Yake, Basi Na Michikichi Yako Inaneemeka.
Ule Muda Wa Kuchimba Karanga Ukifika, Hapo Michikichi Inafurahi Zaidi.
10
 
Nashukuru mkuu, sasa mwaka wa tatu unaanza kupata kiasi gani cha mafuta kwa mwaka mzima, sijapata tafiti ya kutosha maelezo.huko kijijini kwenu kama ardhi ni ndogo hamia mkoa mwingine, tafiti za kikimo zinaonesha katavi chikichi zinaweza kustawi urambo nk, na huko ni maeneo bado yenye ardhi kubwa japo kilimo kama hicho bado watu hawajafunguka.
 
Back
Top Bottom