Msaada wa kimawazo katika hili

Joyce wohwoh

Member
Joined
Sep 17, 2021
Posts
80
Reaction score
185
Wanajukwaa naombeni msaada kwenye hili, nimeagiza gari japan na nimetumiwa profoma invoice na details za kibank kwa ajili ya kulipia inasema tarehe ya mwisho kulipa ni tarehe 9/8/2023 kwa saa za japan.

Nimekwama hapa bank nnayotumia mimi leo nanenane hawafungui ina maana mpaka kesho ndo wanafungua,na japan wako mbele masaa yao zaid yetu, nahsi ntakuwa nje ya mda.nifanyeje?

Niwaambie waniongezee muda? Na wamesema nisipolipa mpaka tarehe walotoa watanireport naombeni ushauri wenu wazoefu
 
Wasiliana nao kuhusu tarehe kupitia njia uliyotumia mwanzo, Wakileta story nyingi Bora uangalie upande mwingine
 
Payment Huwa na option waambie waiforwad utalipia kesho today ni farmers day.
Ungekuwa Dar au Kilimanjaro ungelipia airport kule huduma ni msaa 24.
Hata magufuli stand inafaa huduma za kibenk ziwe masaa 24.
 
Wapigie upesi DP World watakutatulia.
 

Hakuna kitu kama hicho

Mimi nmeagiza gari miezi miwili iliyopita SBT

Hakuna sehemu nlifosiwa kulipa,
Wao usipolipa wanarudisha gari sokoni basi

Ni kampuni gani iyo??

Nashauri usifanye haraka kulipa!!!!!!

Jiridhishe upya!!!
 
Hakuna kitu kama hicho

Mimi nmeagiza gari miezi miwili iliyopita SBT

Hakuna sehemu nlifosiwa kulipa,
Wao usipolipa wanarudisha gari sokoni basi

Ni kampuni gani iyo??

Nashauri usifanye haraka kulipa!!!!!!

Jiridhishe upya!!!
Real motor japan.wameniambia if you do not pay by the due date hiyo tarehe 9 we will suspend your account.
 
Imetumwa leo,nahisi wataireport account yangu kwamba ni tapeli.
Waangalie vizuri maana inawezekana wao ndio matapeli. Wafanyabiashara wa uhakika hawatoi vitisho vya aina hii ili kulazimisha kulipwa. Watakushitaki vipi kwa utapeli wakati gari bado wanalo? Uwe mwangalifu usiumizwe.

Amandla...
 
Waangalie vizuri maana inawezekana wao ndio matapeli. Wafanyabiashara wa uhakika hawatoi vitisho vya aina hii ili kulazimisha kulipwa. Watakushitaki vipi kwa utapeli wakati gari bado wanalo? Uwe mwangalifu usiumizwe.

Amandla...
Sawa fundi itabidi nifatilie account ya bank walonitumia kama ni yao kweli.
 
Real motor japan.wameniambia if you do not pay by the due date hiyo tarehe 9 we will suspend your account.

Mkuu achana nao

Utalizwa muda sio mrefu

Nenda-Autocom,SBT,TrustJapan,Beforwad,Enhance

Huko sijawahi kusikia vitisho

Personaly nawaamini SBT kuliko makampuni mengine coz nliagiza kwao bila hata kupitia agent na nmepokea gari yangu ikiwa katika excellent condition na ntawarecommend tena na tena!!
 
Kwa ushauri tumia SBT au BEFORWAD mimi nakumbuka niliomba Mhindi aniongezee siku 3 mbele na huwa ni waelewa na kabla ya hapo nisha reserve sana gari hadi due date inapita na wala silipi na sijakuwa reported kokote kuwa makini boss tuliza akili unapotaka kufanya malipo na unapochagua gari katika hizo website.

Nakumbuka nilishaikagua gari kwenye picha ni kali ila nikasema hapa nahitaji kujiridhisha zaidi nikamtafuta Mhindi nikamuomba picha na nikamwambia niambie ukweli kama ina dents au scratch yeyote nipe taarifa mapema ni kweli jamaa akaniambia na akatuma picha ambayo inaonyesha scratch ila ukiangalia kwenye website hakuna hiyo picha.

N.B; Omba picha kutoka nje ya website yaani kupitia whatsapp namba zao na waambie wakwambie ukweli kuhusu changamoto yeyote ya hiyo gari usiwe na haraka ya kulipa.​
 

Sahihi kabisa
Rule no1.Usiwe na haraka

Mimi ilichukua 6working days kupata chuma nayotaka
-leather seats
-memories heated seats
-sports rims
-body kits
-low mileage
-and cheap prices[emoji23]

Nlikomaa na mjapan mpk akanipa tricks
Mojawapo akanambia achana na hizi zilizopostiwa
Kila alhamis kuna auctions tunachukua gari mnadani
So by ijumaa/jmosi tunazipost akanipa na muda akasema pale utapata bei rahisi na huwa hazikai kabisa

Kweli bana
Nlishaangaa tu Chuma 2 zmekuja tena hata picha hazifunguki vizuri lkn details mulemule nka-reserve chap

Usikurupuke take your time usiogope kumuuliza mjep
 
Shukrani mkuu kwa mawazo,japo nimekata tamaa kabisa ya kuagiza hakuna dola kwenye bank zote na hawakubali TT transfer toka asubuh natafuta imebidi sasa nirudi tu home kusubiri itakuwaje naombeni ushauri.nasikia beforward unaweza lipa kwa Tz shillings kwenye account yao ya Tz?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…