Msaada wa kimawazo: Nahisi naanza kupata depression

Lengo la kuoa ni kupata mtoto, ushapata unataka nini tena?
Usioe mwanamke mwenye pressure za kuolewa. Ndoa inakuja automatically tu. Wewe mwenyewe from no where u will feel like its the right time. Hutaambiwa wala kushawishiwa na mtu.
Sasa jilipue uone balaa baadae
 
Umri sahihi wa mwanaume kuingia kwenye ndoa ni kuanzia 35...hapo akili inakuwa imekomaa vya kutosha, ujinga mwingi pia unakuwa ushamtoka,hivyo anajitambua kwa maana halisi ya kujitambua
Kabla ya hapo ni muhimu sana kutokubali ushauri wa VUA KONDOM ama LEO TUSITUMIE KINGA NIKO SIKU SALAMA

Ushauri mwingine kwa wadogo zangu wa kiume CHUKUA TAHADHARI kubwa sana siku mpenzi wako anapokulazimisha mkalale tena bila kinga
 
....Mtoto najua ni wangu coz tunafanana sana, kachukua kila kitu kwangu.
Dogo, nikafikiri labda ulibambikiziwa mimba, kumbe sivyo!

Sasa kama mtoto ni wako depression ya nini?!!!

Ushalamba asali huwezi kujizuia tena.. Ukiacha huyo fasta utachukua mwingine. Muda si mrefu utakuwa na timu nzima ya watoto bila mama zao kwa kisingizio hicho hicho🙄
 
nilichokupendea ulimweleza ukweli huna mpango wa kumuoa akaamua kujitegea ili aipate ndoa yan aolewe kisa ana mtoto wako, ndugu usilazimishwe ndoa hailazimishwi wala haifanywi kwa sababu tu kuna sababu ipelekeee ndoa,

waambie ukweli wazazi wako,waambie hayuko moyoni kuishi naye ni sawa na kumtesa kihisia na kumpunguzia mzigo lea mtoto wako tu wewe endelea na maisha yako

huyo dada hana akili yan uelezwe ukweli ukaitegeshe mimba ili tu uolewe? ndoa ni taasisi pana yataka muwe mmekubalia kwa pamoja sasa tunaenda kuanzisha maisha yetu sio hivyo haitadumu,

simamia moyo wako unavyokusukuma.
 
Hivi we unajua depression kweli? Sema tu hujajipanga usilete excuse za depression, wakati unakwichikwichi kavu utelezi ndio utamu wa amri ya sita ulikuwa hujui hayo?

Mwanaume wa kweli hakimbii majukumu

Acha kutafuta huruma ziso na msingi

Mwanaume majukumu, Mwanaume kupambana
 
Jamanii mnapata uthubutu upi kukulana na mwanamke/mwanaume dry ambae huna future nae..?? Mnatujazia tuu single parents na watoto kukosa malezi ya pande mbili...bro we pambana tuu na familia yako ndo'basi tena..
 
Na sasa TZ takwimu za talaka zinaongezeka. Marriage in haste repent at leisure.

Tutashauri mengi lakini mwisho ni kwamba the heart cannot be ruled.
 
Umenena vizuri sana mkuu
 
Ukibahatika kupata kazi nje ya huo mkoa, nenda. Ukiwa mbali vitu vitaa kwenye perspective na utajua unataka nini. Now upo ndani ya box. Kila.kitu kinakua kigumu
 
Maisha bhana
Tambua ujikuta umependa usipopendwa
 
Si kila wakati mambo yataenda kama vile tunavyotaka yawe.
Kwani ana kasoro gani ambayo unahisi itakuwa kikwazo kuwa mke wako? Kipi hasa unaona kinakuzuia usioe kwa sasa?
Mtazame mwanao then fanya maamuzi sahihi kwa ajili yako na yake.
Binafsi sipendi na wala sitarajii kuwa na watoto kwa mama tofauti. Familia mzuri ni ile mnakuwa pamoja. Wazazi na watoto wa pamoja. Bila mwingiliano sijui huyu mama yake fulani haipendezi.
 
Miaka 35 kushuka chini mapenzi yatawatesa sana nakuwaharibia.maisha kilasiku tunawambia muwe namahusiano na watu wenye sifa zakuoa inawezekana hujui sifa zamwanamke wakuoa
 
Kuna sehemu jamaa kasema hampendi mwanamke? Jamaa tatizo lake ni muda wa kuoa anaona bado haujafika
 
Huo ni mtego... angalia usije kufilisika ukakimbiwa
 
Mimi pia niliwahi tokewa na hilo ila nililipokea na nikakubali japo mwenzangu yupo mbali kikazi ila nilimpokea. Hivyo usichukue maamuzi mabaya fungua moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…