Msaada wa kisaikolojia

Msaada wa kisaikolojia

Alan Madiga

Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
26
Reaction score
2
WanaJF, nimeishi kwa miaka ishirini na sita (26) sasa nikiwa nimepoa moyo kabisa. Sina hisia za upendo na sijawahi kuhisi hivyo toka mwaka 1996 nilipokuwa darasa la pili.

Nakumbuka mwaka huo nilikuwa darasa la pili na tulikuwa tunaishi kota, enzi zile shule tulikuwa tunatoka saa nne asubuhi.

Nyumbani nilikuwa nashinda na mfanyakazi wa kike wa jirani yetu.

Huyo mdada alikuwa ni mtu mzima tayari na alikuwa akinifanya mimi kama mpenzi wake. Kwa umri niliokuwa ilikuwa ngumu kujua kama nilikuwa nabakwa wakati huo na nilitumika kumridhisha huyo binti pasi na kujua lolote.

Haikuishia hapo kuna likizo moja mimi na mama yangu tulikwenda kumtembelea bibi kijijini. Huko ilinitokea hali hiyo ya kutumiwa kimapenzi na mama yangu mdogo. Hii iliniumiza sana kuujua utupu wa mama yangu mdogo nikiwa bado mdogo sana na sikujua ananitendea jambo gani.

Sasa nimepevuka na najua mema kwa mabaya. Nilijaribu wakati ule kusema lakini hakuna aliyekuwa tayari kunisililiza vile wazazi walikuwa bize na shughuli zao.

Ili nijengea hali ya uoga na kutojiamini mbele za watu hivyo ikanifanya nianze kujitenga na kuwa mbinafsi kadri ninavyokua.

Hakuna aliyejali kuhusu mimi kwa nini mimi nijali kuhusu wao?

Nilipo barehe na kuanza mahusiano ya kimapenzi na wasichana, kuna hali ya roho ya ukatili na kisasi inanitawala mpaka nashindwa kudumu na msichana yoyote yule.

Naona hakuna binadamu mwenye kujali shida za mwingine zaidi ya kila mtu kujali kutimiziwa haja zake tu. Nimejitumikisha ktk hali ya kulipa kisasi na kujiridhisha nafsi yangu kwa zaidi ya miaka 15 lakini bado sijaweza kupata ahueni ya kisaikolojia ili nisahau vitendo vya kubakwa utotoni.

Nimewaumiza wengi na sasa nimechoka na nahitaji msaada wa matibabu ya kisaikolojia ili niweze kupenda km wengine wanavyopenda ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi na maisha.

Nawakilisha.
 
Pole kwa unayoyapitia naelewa unachokiongelea na naelewa maumivu uliyonayo.Pole kwa kuhusishwa na masuala ya kikubwa kabla ya umri wako.Njia pekee ya kuepuka hali hio ni kuwasamehe hao wabakaji na walawiti wa watoto kwani hawajui makosa yao.Naamini mtu kwenye akili timamu hawezi kutenda waloyatenda hao.Usitumie background yako ya maisha kujenga ufa kwenye mahusiano yako ya sasa.Kumbuka wewe ulikuwa muathirika na hukuwa na usemi juu ya maovu uloyapitia lakini sasa una sauti,unaweza kuitumia sauti hio.Njia mmojawapo ya kuepukana na adha hio ni kuongea na wahusika face to face ili wajue makosa yao na wasiyarudie tena na nakuahidi wataaibika sana na kufedheheka.Bila shaka walikuona mtoto na wakajua hutokuja kukumbuka haya ukubwani na hawakuwa na ujuzi wa athari gani wanazokupandilia lakini watoto wanakumbuka mengi mno.
Ukiwa kwenye mahusiano kuwa muwazi na uongelee kuhusu maisha yako ya awali ili mwenza wako apate uelewa juu ya yale uloyapitia.Mueleze kwamba upo emotional unstable,una low self-esteem,depression, upo anti-social kama matokeo ya matendo hayo.Akikukubali wewe kama ulivyo utajenga imani nae na inatasaidia kudumisha mahusiano yenu.
 
you can learn to love quite well!cha kufanya anza na tamhiliya za kifilipino,wasamehe waliokukosea,soma vitabu vya mahusiano,mapenzi na saikolojia!fanya hivyo na ulete feedback!
 
Samehe na uwaachilie waliokuumiza .
Nafsi zetu zina masikio na macho ongea na nafsi yako kwa kumaanisha kuwa umechoka kutumikishwa na roho za kisasi unataka kupenda kama ambavyo binadamu wengine wanavyopenda.
Najua utakuwa na vigezo vyako katika kumpenda mwanamke utampata na utenjoy.
Lakini kubwa kabisa ni kusamehe na kuwaachilia hao watu ulio washikilia
 
Alan najua unaamini katika Mungu mwambie ashughulike na mambo yako lakini jiachilie wewe kwanza kakangu! kwakusamehe na waangalie wanawake katika mtazamo chanya.
 
La kwanza na la muhimu mno ni kuikubali hiyo hali, na kuichukulia kuwa yalikuwa ni mapito halafu cha pili ni kusamehe na kuanza upya kumbuka hawa unaowaumiza sasa hawana chembe ya kosa bali ni wahanga wa jinsia
Vilevile kuna watu udogoni mwao walitendewa mabaya kuliko wewe, wao walilawitiwa na ndugu wa damu, halafu pia jifunze kuwa wewe lakini usiwe katili kuna mengi mazuri na wengi wazuri ambao hawapaswi kuwa wahanga wa matendo ya wengine
Kwa kuwafanyia ukatili unaendeleza ile roho kwakuwa wao walijitoa kwako kwa upendo mkuu lakini ukawaumiza nao wataenda kuumiza wengine
 
Nashukuru sana kaka. Yule wa kwanza sijui yuko wapi lakini najua ameshaolewa na anaishi raha mustarehe. Mama mdogo yupo na ameshaolewa na ana watoto wanne japo hawezi kunitazama usoni kabisa.
 
you can learn to love quite well!cha kufanya anza na tamhiliya za kifilipino,wasamehe waliokukosea,soma vitabu vya mahusiano,mapenzi na saikolojia!fanya hivyo na ulete feedback!

Hiyo nilijaribu na ilisaidia kidogo lakini siyo kuondoa hasira zote. Nitafanya tena mpaka nikae sawa.
 
Alan najua unaamini katika Mungu mwambie ashughulike na mambo yako lakini jiachilie wewe kwanza kakangu! kwakusamehe na waangalie wanawake katika mtazamo chanya.

Hapo ndio pagumu kuanza kuwatazama kwa mtazamo chanya coz hali mbaya inanishinda na siwezi kuicontrol kabisa na nakuwa mkatili kiliko ninavyoonekana kwa watu.
 
La kwanza na la muhimu mno ni kuikubali hiyo hali, na kuichukulia kuwa yalikuwa ni mapito halafu cha pili ni kusamehe na kuanza upya kumbuka hawa unaowaumiza sasa hawana chembe ya kosa bali ni wahanga wa jinsia
Vilevile kuna watu udogoni mwao walitendewa mabaya kuliko wewe, wao walilawitiwa na ndugu wa damu, halafu pia jifunze kuwa wewe lakini usiwe katili kuna mengi mazuri na wengi wazuri ambao hawapaswi kuwa wahanga wa matendo ya wengine
Kwa kuwafanyia ukatili unaendeleza ile roho kwakuwa wao walijitoa kwako kwa upendo mkuu lakini ukawaumiza nao wataenda kuumiza wengine

Mi nimechoka hali hii lakini hisia mbaya zinanikaba sana.
 
Samehe na uwaachilie waliokuumiza .
Nafsi zetu zina masikio na macho ongea na nafsi yako kwa kumaanisha kuwa umechoka kutumikishwa na roho za kisasi unataka kupenda kama ambavyo binadamu wengine wanavyopenda.
Najua utakuwa na vigezo vyako katika kumpenda mwanamke utampata na utenjoy.
Lakini kubwa kabisa ni kusamehe na kuwaachilia hao watu ulio washikilia

Natamani sana kuwa na mahusiano lakini hakuna anayeweza kunielewa.
 
Find a woman doctor ajue tatizo lako halafu anzisha nae mahusiano...itakuwa easy for you to heal
 
Kutojiamini na uoga mbele za watu ni hali inayosumbua wengi sana,siyo wewe peke yako.Wana JF wekeni solution threads za uoga na kutojiamini ili watu wapone!
 
mmh pole sana alan,kusamehe na kujaribu kuyachukulia yalikuwa ni mapito tu itasaidia,pia ungepata cancellor ikiwezekana wa dini coz naamini kwa mungu hakuna linaloshindikana,cha mwisho usione kama tatizo lako ni kubwa sana kumbuka kuna wenye matatizo zaidi hata ya kwako
 
Duh! Ndugu usije ukawa unatumia kubakwa kwako kama sababu ya kuwaumiza watoto wa kike.Mimi sioni kama kubakwa kwako kunaweza kuwa na athari kiasi hicho kwako,watoto wa kike ndio huwa wanaathirika sana kwa hilo ila sio wa kiume,by the way ulikuwa mtoto na ulikuwa hujui kinachoendelea so inakuathiri vipi?

Nina marafiki zangu wawili ambao waliyajua mapenzi wakiwa wadogo kupitia kwa house girls na haijawahi kuwa athiri kiasi hicho.Sitaki kuamini kuwa wao ni tofauti sana na wewe kiasi kwamba wewe ikuathiri kiasi hicho.

Wewe hiyo chuki umeijenga kwa kupenda mwenyewe na ni tabia yako ya umalaya ndio inakufanya usipende not otherwise.Its not a psychological problem,acha umalaya chagua mmoja kati ya hao utulie naye.
 
xfactor nadhani unaelekea kuwa na familia au tayari unayo. Natumaini wanao utawatunza vyema na kwa Usalama lakini jaribu kumtafuta mtaalamu wa saikolojia akuelimishe hali ninayo pitia mimi sasa. Sihitaji kutimikia hali ya. kikatili na naamini kuna mengi sana yamejificha kwenye jamii zetu licha ya matukio yanayo tangazwa mara chache. Jiulize kwa nini upendo wa watu umepoa? Watoto wanasikilizwa na kuhudumiwa inavyopaswa? Nani anapaswa kumfanyia ubaya huu mwenzake? Kuna mengi nataka kusaidiwa hapa lakini siyo mawazo finyu km yako xfactor.
 
Duh! Ndugu usije ukawa unatumia kubakwa kwako kama sababu ya kuwaumiza watoto wa kike.Mimi sioni kama kubakwa kwako kunaweza kuwa na athari kiasi hicho kwako,watoto wa kike ndio huwa wanaathirika sana kwa hilo ila sio wa kiume,by the way ulikuwa mtoto na ulikuwa hujui kinachoendelea so inakuathiri vipi?

Nina marafiki zangu wawili ambao waliyajua mapenzi wakiwa wadogo kupitia kwa house girls na haijawahi kuwa athiri kiasi hicho.Sitaki kuamini kuwa wao ni tofauti sana na wewe kiasi kwamba wewe ikuathiri kiasi hicho.

Wewe hiyo chuki umeijenga kwa kupenda mwenyewe na ni tabia yako ya umalaya ndio inakufanya usipende not otherwise.Its not a psychological problem,acha umalaya chagua mmoja kati ya hao utulie naye.

Sitaki umaarufu hapa ninachotaka ni msaada na uchambuzi wa hali yangu ili wasioweza kupaza sauti zao hadharani wajue nini cha kufanya ili kujikomboa kutoka ktk hali km yangu.
 
Natamani sana kuwa na mahusiano lakini hakuna anayeweza kunielewa.
Kwanini unakuwa na mtazamo hasi kwanini unaamnini hakuna atakaye kuelewa ? Je ni kwasababu ya unawamistreat?
Kataa hiyo hali acha kumtukuza ibilisi
 
Back
Top Bottom