Ninachojua mimi kazi ya mwanasheria unapomuita katika mauziano ya vitu ni
1. Kufanya tafiti na kujua uhalali wa kumiliki na uhalali wa kuuza wa eneo au nyumba husika.
2. Kuandaa nyaraka za mauziano kisheria.
Nionavyo hapo wakili hakufanya kazi yake na ikibidi mfungulie kesi mahakamani ili akufidie yeye au Bima yake.
Kwa hapo alishindwa kutekeleza jukumu lake la kwanza kwa weledi au kwa maslahi binafsi, Aliyekuuzia nyumba (mdogo wa marehemu) sio mtu sahihi ni lazima Angekuwa msimamizi wa miradhi au kungekuwa na mhutasari wa kikao cha familia kuridhia kufanya hiyo biashara.