Msaada wa kisheria je nimechukua hatua stahiki au nimejifunga mwenyewe?

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Mimi ni wakala wa m-pesa hapa mtaani wapo mawakala wenzangu kama yetu huwa tunaaminiana kama mawakala maana miongoni mwa sifa kuu ya kuwa wakala ni uaminifu. Sasa ipo hivi kuna siku nilikosea kutuma pesa kwa njia ya froat nikajikuta nimemuwekea wakala mwingine lakini ni jirani pia. Haraka nkamfuata na kumweleza hivyo akanijibu ndio atanipa baadae pesa kiasi cha 150000/=asubuhi yake huyo kijana hakuonekana tena.

Nikachukua uamuzi wa kwenda na wakala mwenzangua akioneshe kwa bosi wake
Baada ya kufika kwa bosi akaeleza kua jana ndo alikua anakabidhi ofsi na kansababishia losi ya karibia laki 1.na ameenda kusikojulikana kwa hio nikimpata ntawajulisha.
Imepita ck nzma bila kunijulisha nami tarehe hiohio 5 nkapiga cm voda wakazuia pesa yangu na pia nkaenda polisi kulipoti juu ya kutapeliwa na huyo kijana nikapewa RB ya kunilinda.
Leo yule bosi kaenda kwa dean of student kuniripoti kua nimekula njama na kijana wake akatoroka, baada ya mimi kuitwa na kutoa maelezo na ushahidi wa msg iliyomuahamishia pesa kimakosa ikoenekana mimi nina ushahidi ila yule jamaa hana ushahidi, ameomba barua ya kwenda central police ili mimi nikamatwe kwa utapeli na pesa yangu tayari wameirudisha leo na RB ninayo kabla yake japo yeye hajui.

Je hapo ntaweza shinda kesi au ninasubiri kutiwa pingu. Na je RB yangu inaweza kutumika kama ulinzi wangu? Huyu dada anadai ninajua huyo kijana alipo maana nnajuana nae, je hii inanitia mimi hatiani?

USHAURI WENU NA MSAADA WA KISHERIA ILI NISHINDE KESI HII.
 
wacha woga. wewe eleza ukweli wako tu. atathibitisha vipi kuwa unajuwa alipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…