Msaada wa kisheria juu ya hii kesi

Dj-kobo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
458
Reaction score
193
Wakuu habari ya majukumu,

Wakuu msaada wenu kwenye hii kesi ni muhimu sana kesi yenyewe ni ya Kiwanja , ambapo mzee huyo alinunua kiwanja kwa bei halali na baadae akawa na nakala za umiliki wa Kiwanja.

Baadae aliyemuuzia akaenda kushtaki Baraza la Ardhi la Kata kesi ikaamuliwa katika mazingira ya rushwa na alieshtaki yaani muuzaji wa kwanza akaonekana ameshinda kesi.

Aliyeshindwa ambae ndo mnunuzi akakata Rufaa kwenye Baraza la Ardhi la Mkoa na katika baraza hilo mkoani rufaa ikaamuliwa kua yule mnunuzi ana mamlaka ya kumiliki kiwanja na hana sababu ya kukirudisha.

Sasa ofisi ya Mkuu wa Wilaya imemwandikia barua yule mshindi wa Rufaa apeleke vielelezo vya umiliki wa ardhi ile hii imekaaje.
 
kwanza ieleweke alimshitaki kwa madai yapi.na wakati wa mauziano nini waliandikishanaje.kuombwa vielelezo ni sawa maana lazima.wawaulize wote wawili.hapo naona kuna kitu ndan yake busara ni kusikiliza pande zote mbili.si rahis kusema kunavmazingira ya rushwa bila kujua mchakato wa mauziano na makubaliano ulikuwaje.usipojar nipm kwa msaada zaidi
 
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya haihusiki kwa namna yoyote na mashauri ya ardhi. Anachotakiwa kufanya mhusika ni kutowasilisha vielelezo vyovyote kwa Mkuu wa Wilaya.

Asiyeridhika afuate taratibu za kimahama. Asiyeridhika akate rufaa Mahakama Kuu,Kitengo cha Ardhi. Kumsikiliza Mkuu wa Wilaya katika hili ni kukaribisha siasa na ubabe katika masuala ya kisheria.
 

Mkuu land division bado ipo?
 
Mkuu land division bado ipo?

LAND DIVISHENI bado ipo sana. Watu wengi, wakiwamo mawakili wanaconfusi sana hapa. Land Divisheni ilianzisha na High Court Registry Rules, GN 63/2001 chini ya Judicature and Aplication of Laws Act. Hiyo sheria wanayodhani ilifuta Land divisheni ya High Court (Act No 2 of 2010) haikufuta, bali ilitoa jurisdiction kwa mahakama kuu zote kusikiliza masuala ya ardhi. In other word, the Land Division of the high court is a creature of statute and can be disestablished by a statute only. act no. 2 of 2010 cannot establish or disestablish a registry, subregistry or a division of the high court. Authority pia zipo
 

Thank you Learned Brother.
 

Sikuimanisha hiyo sheria ya 2010 ila kuna sheria ya 2013 inayofuta land divisions. Kama hzo kesi zipo tunaomba hata citations
 
Sikuimanisha hiyo sheria ya 2010 ila kuna sheria ya 2013 inayofuta land divisions. Kama hzo kesi zipo tunaomba hata citations
nakubaliana na permanides. Sheria na 2 ya 2002 ilishafanyiwa marekebisho ambapo neno land division limeondolewa kila mahali panaposomeka high court land division
 
dj kobo. silaha yako kwa sasa kwenye suala hili ni maamuzi ya baraza la ardhi na nyumba wilaya. suala la kupeleka nyaraka kwa mkuu wa wilaya hiyo sio forum sahihi ni kuwa makini nayo sana.
 
kama mtu amepewa haki na mahakama njia pekee ya kupinga ni ya mahakama yenyewe, mkuu wa wilaya hawezi kuhoji maamuzi ya mahakama kama mamlaka. kufanya hivyo ni kunaleta muingiliano wa mamlaka kati ya mihimili miwili yaani executive na judiciary. kitu ambacho hakiruhusiwi kisheria. huyo mtu hana haja ya kupeleka vielelezo ila ni kusubiri hatua yoyote mkuu wa wilaya atakayo chukia ili aka lalamike court.
kuhusu land division namimi nilikuwa najua kuwa kilichotoke ni kuipa high court general division mamlaka ya kusikiliza kasi za ardhi. ila kama kuna mababiliko ya sheria recentry wekeni hapa yufuatilie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…