Msaada wa kisheria juu ya malipo ya mstaafu jeshi

Mwimbe CL

Senior Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
147
Reaction score
96
Ndugu wana jukwaa,

Nahitaji msaada wa kisheria kwa hatua za kufuata baada ya mama yangu kuzungushwa na kulipwa kidogo.

Kwa mujibu wa maelezo yake anatakiwa kulipwa 470,000 kila baada ya miezi mitatu. Lakini kila miezi mitatu ikifika inaingia Mara 100,000.Mara nyingine 150,000 na kuna kipindi hawakuingiza chochote kwa miezi 6 akafatilia akaambiwa ahakiki taarifa zake pesa zitaingia, lakini baada ya kuhakiki Hazina wakamwambia pesa imeingia akaenda bank akaambiwa imeingia lakini haija Open.Hivyo hawezi kuitoa kila akienda anajibiwa hivyo.

Naombeni msaada wa hatua zipi azifuate ili alipwe stahiki zake zimsaidie kujikimu kimaisha.

Natanguliza shukurani zangu za dhati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…