Msaada wa kisheria juu ya mgogoro wa ndoa

Msaada wa kisheria juu ya mgogoro wa ndoa

Gefu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
6,930
Reaction score
2,565
Salaamz,

Yupo mama kaniomba ushauri juu ya ndoa yake, nami nimeona suala limekaa kisheria zaidi, hivyo naomba ushauri/msaada wa nini kifanyke. Mama huyu ana mgogoro wa ndoa yeye na mmewake(hawajatengana), mwanaume kaamua kuokota kabinti mtaani anatembea nako. Imefika mahali huyo mzee kaanza kuuza mali alizochuma pamoja na mke wake wa ndoa na kwenda kutumbua na mke wake mpya. je sheria inasema nini juu ya jambo hili, mke anahaki ya kwenda mahakamani kupinga uuzwaji wa nyumaba ? na je mume ana mamalaka kisheria kuuza mali yoyote waliyochuma na mkewake pasi kumshirikisha mkewe. kama inatokea hivyo hatua gani zichukuliwe kwa mke kupata haki yake. je kuna vituo vya msaada wa kisheria vya kuweza kumsaidia huyu mama..? muongozo tafadhali...asanteni..
 
...wadau mbona kimya sana, au wote sheri haijakaa sawa kama mimi, hata msaada wa mawazo jamani tumsaidie mdau mwenzetu..
 
Mwanamke ana haki ya kupinga uuzwaji wa mali walizochuma wote, ila kifupi mwambie aende TAWLA watamsaidia sana.
 
aende TAWLA kweli,aende jumatatu,watamsaidia vizuri
 
..lazima jumatatu au kwakuwa leo ni ijumaa, wikiend hawafanyikazi...?

kwa ninavyojua,msaada wa kisheria wanatoa every j3 na j5 tu,saturdays hawafungui ofisi.
 
kwa ninavyojua,msaada wa kisheria wanatoa every j3 na j5 tu,saturdays hawafungui ofisi.

...thanks ngoja nimshauri,ofisi zao zipo wapi...?
 
Hapo kifungu cha 114 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kinahusika...hizo ni mali za joint efforts, na hata kama mke hana mchango wa moja kwa moja, bado ana haki katika hizo mali, na kuuza lazima ashirikishwe
 
...so case inaanzia primary court moja kwa moja ? na kesi inafunguliwaje ya madai...au inakuwaje mkuu..
 
Kabla ya kufungua kesi mahakamani wanandoa lazima waende kwenye Mariage Conciliation Board kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 101 cha sheria ya ndoa ya mwaka 2002 unles there is exception hard ship as per Section 100(2) of The Law of Marriage Act as amended in 2002.
 
As per Section 101 of the Law of Marriage Act,the party must refer to the Mariage Conciliation Board before filing a case to a competent court unles there is exception hard ship as per Section 100 of The Law of Marriage Act as amended in 2002.
 
...so case inaanzia primary court moja kwa moja ? na kesi inafunguliwaje ya madai...au inakuwaje mkuu..

Mahakama ya Mwanzo, Hakimu Mkazi, na Mahakamu Kuu zina uwezo sawa katika mashauri ya ndoa. Anaweza kufungua kesi ya madai Mahakama ya Mwanzo
 
As per Section 101 of the Law of Marriage Act,the party must refer to the Mariage Conciliation Board before filing a case to a competent court unles there is exception hard ship as per Section 100 of The Law of Marriage Act as amended in 2002.

Mkuu hapa umeenda chaka. Kifungu cha 100 hakizungumzii hayo. Kinazungumzia divorce.
 
Mwanamke ana haki yake pia katika malio walochuma wote hata kama almkuta mwanaume anayo tayari,lakin kwa namna moja ama nyingine nguvu ya mwanamke imetumila pia kuendeleza rasilimali hiyo.hujasima yupo wapi,kama yupo dar anaweza kwenda pale WLAC,pale karibu na kituo cha daladala manyanya aulizie kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake,wapo kwa ajili hiyo hasa.kama yuok mikoani aulizie kituo cha NOLA kilichopo karibu nae.
 
Back
Top Bottom