Nataka kupata nafasi ya kuingia magereza (yoyote) ili niongee mawili matatu na wafungwa na kupublish mahojiano hayo, je ni hatua zipi za kisheria natakiwa kufuata ili kuwa na uhalali wa kufanya hivyo?...
Kisheria huwezi, sababu hakuna sheria au utaratibu unaoruhusu hicho kitu kwa mtu binafsi, isipokuwa wanaoruhusiwa kuingia gerezani na kuongea na wafungwa ni tls yan chama cha wanasheria, na hawa wanafanya mara moja tu kwa mwaka yan desemba 16 zile siku 16 za ukatili wa kijinsi zikishapita ndio inadondokea siku ya haki za binadamu sasa baada ya pale secretariet ya tume ya ushauri wa kisheria yan LAS hawa ndio wanatangazaga kwenye tv kuwa chama cha wanasheria watatoa msaada magerezani katika tarehe iliyopangwa nchi nzima na kila mkoa wanasheria huwa wanaenda. Na hapo hawaingii na simu wala chochote kile zaid ya kuongea na wafungwa na kuandika ma file kwa walichoona. Hakuna mwandishi anayeingia wala nini. na wanasheria wanakaguliwa vibaya mno, sisi tuliandika barua kwa kamishna kuomba kuangalia tu bila kufanya chochote ndio tukaitwa na kupewa somo hilo. Ingawaje taasisi yetu imesajiliwa kutoa msaada wa sheria lakini bado hatukuweza kuingia.