Msaada wa kisheria katoroshwa na ndugu zake na mtoto

Msaada wa kisheria katoroshwa na ndugu zake na mtoto

mshana org

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2012
Posts
2,091
Reaction score
619
Wanabod habar za majukumu.kwanza nitangulize shukran kwa msaada wanaopata watu humu kuhusiana na maswala haya ya kisheria.nakuweza kupata muongozo wa kutatua matatizo yao.
Mimi nina ndugu yangu yeye na mkewe hivi mwezi ulopita ndoa yao iliingia dosar kwa jamaa kufumwa na sms za mwanamke na mkewe.jamaa alijitetea lakin mke hakuelewa akakimbilia kwao.jamaa akaenda wakaekwa kikao na wazee lakin mke hakuelewa akasema apewe muda afikirie akiwa kwao.kesho yake ndugu zake wakamchukua na kwenda kuish nae mkoan bila jamaa kujua kinachoendelea baada ya wiki ndo anakuja kujua kumbe mke hayupo kaondoka na mtoto na akiwapigia shemeji zake pamoja na wakwe zake hawampi majibu yanayoeleweka.mtoto wao ana miaka miwili na nusu.hii inaonekana ndug zake hawataki warudiane.sasa jamaa anataka mwanae kama itashindikana mke kurudi je ataweza kumpata kisheria?na kama inawezekana ni njia gani anaweza kutumia na afungue kes ya aina gani.naombe tumsaidie ndugu yetu
 
Hii noma ila mtoto wa miaka miwili hapewi ng'oooo
 
Sasa kama hapew na mtoto hajulikan yupo kwenye usalama gani inakuaje
 
Hii noma ila mtoto wa miaka miwili hapewi ng'oooo
...siyo kweli kuwa mtoto WA miaka miwili hapewi ng'oo, Kuna kitu huwa watu wengi hawaelewi kuwa sheria huwa Ina msimamo mkuu (general rule) Na mbadala wa huo msimamo (exeption)
Kweli sheria inaelekeza mtoto atalelewa na mama mpaka afikishe umri wa miaka 7, ikiwa wazazi wametengana, lakini zipo sababu za msingi kabisa ambayo baba ataruhusiwa kupewa mtoto endapo ataweza kuiridhisha mahakama Ni kwa nini apewe mtoto ambaye hajatimiza miaka 7. Kumlea.
 
Kwa issue yako ipo hv,
1. Fahamu mahakama ndo chombo pekee kinachotoa talaka.
2. Suala la mtoto aishi Na nani Ni mpaka kuwepo Na talaka, yaani mahakama itambue kuwa ninyi wawili mmetengana, kwa huwezi kujadili suala la mtoto aishi na nani Kati yenu kisheria ikiwa mahakama bado inatambua kuwa ninyi Ni mke Na mme.
3. Hivyo ukitaka kumpata mtoto kisheria ni mpaka mtalikiane, hivyo wewe ufikirie kuwa Kama ninyi wawili mmefikia hatua ambayo hawezi tena kuishi pamoja, hapo upeleke ombi la talaka mahakamani, Na katika ombi Hilo ndiyo utazungumzia sababu za kupewa mtoto. Kumbuka Ni lazima uwe Na hoja za msingi Ili kuiridhisha mahakama kwanini upewe mtoto.
4. Kumbuka general rule Ni kuwa mtoto atalelewa Na mama mpaka atakapo fikisha miaka 7.

Natumaini umepata mwanga.

Maelekezo haya Ni kwa mahsusi kwa suala lako Tu, Na siyo msimamo wa sheria. Hivyo unaweza tafuta wakili akakusaidia zaidi.
 
Mtoto atakuja mwenyewe akikuwa. Na mke aoe mwingine kama hali ikiruhusu.
 
Nasikia sasahiv ndugu wa mke wamemchukua ndug yao na kwenda kuish naye mkoa kibaya zaid jamaa akipiga sim hata kujua hali ya mtoto wake hapew majibu ya kueleweka.
 
Back
Top Bottom