Msaada wa kisheria kuhusu Ardhi

Msaada wa kisheria kuhusu Ardhi

Dalali wa mjini

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2024
Posts
326
Reaction score
464
Habari wakuu.

Kuna mhusika ana eneo lake ukubwa ni heka moja Kwa vipimo vya macho lakini ndani ya Hilo eneo Kuna nguzo ya umeme laini kubwa ile ya 33.

Sasa anataka kupeleka wataalamu wa Ardhi kwajili ya kupima ili kuweka mawe ya Ardhi (Bikoni). Gharama zimekaaje hapo wakuu na Je anaweza akapimiwa kiwanja chake ikiwa umeme mkubwa umepita.

Hili eneo lipo mjini kabisa Buza kwa lulenge na kuna nyumba 5 ndani ya eneo.
 
Kama Kuna zile nguzo za Umeme mkubwa wa TANESCO jaribu kufanya uchunguzi kwanza isijekuwa eneo Hilo sio lake au lilishakuwa acquired.

Kuhusu gharama awaulize hao wataalam anaotaka kuwapeleka. (Gharama haziko fixed)
 
Kama Kuna zile nguzo za Umeme mkubwa wa TANESCO jaribu kufanya uchunguzi kwanza isijekuwa eneo Hilo sio lake au lilishakuwa acquired.

Kuhusu gharama awaulize hao wataalam anaotaka kuwapeleka. (Gharama haziko fixed)
sehemu kunakopita zile nguzo huwa kuna umbali nadhani mita 15 kila upande kama nitakuwa sijakosea, inawezekana sehemu ya eneo si lake ila kwa kujiridhisha aite maafisa ardhi/mipango miji wanaweza kumpa jibu halisi zaidi Dalali wa mjini.
 
Kwa nguzo ya umeme wa 33kV, hifadhi ya usalama kawaida ni takriban 15 mita kila upande wa nguzo (yaani jumla ya 30 mita kama upana wa ukanda wa hifadhi).

Hata kama eneo hilo litawekwa ndani ya ramani yako, huenda lisiruhusiwe kujengwa au kufanyika shughuli fulani.

So wasiliana na tanesco kitu cha kwanza then watu wa ardhi.
Gharama i guess kwa huko kwa ukubwa huo andaa 400,000mpka 800,000
 
Back
Top Bottom