Junior Hamis
JF-Expert Member
- Aug 31, 2013
- 354
- 294
kuna rafiki yangu alienda kutoa pesa katika ATM za Bank fulani baada ya kuandika kiasi mashine ikahesabu halafu haikutoa kiasi chochote cha pesa halafu card ikarudishwa akaenda bank kuulizia akahisi labda kadi yake ina matatizo lakini bank wakamwambia kulikuwa na tatizo hivyo basi pesa yake kiasi cha shilingi laki 3 itarudishwa kwenye account yake baada ya muda wa masaa 72 akasubiri muda ukafika ila pesa haikurudishwa baada ya kurudi tena bank akaonana na manager wa hiyo branch akamwambia wanashughulikia hilo suala. Sasa ni zaidi ya mwezi na wiki 1 lakini amekuwa akiambiwa kuwa asubiri tatizo linashughulikiwa na ana shida na hiyo pesa.Naomba kuuliza ni hatua zipi za kisheria inambidi azifate kama hiyo Bank wataendelea kumzungusha bila kumrudishia pesa zake ni wapi anatakiwa kwenda na hatua zipi za kuchukua.