masaho
Member
- Apr 29, 2014
- 9
- 3
Nimenunua eneo la ardhi, aliyeniudhia hilo eneo ni mwanaume mbele ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa , kabla ya mauziano hayo niliulizia kuhusu umiliki wa eneo nikadhibitishiwa kuwa ni lake na nikahoji kama ana mke akasema hana mke walikwisha achana zaidi ya mwaka mmoja na walizaa mtoto mmoja na huyo mtoto yuko naye yeye anamlea.
Huyo mwanamke hakumuoa kwa ndoa waliishi tu na maelezo haya niliyathibitisha kwa balozi na majirani hivyo nikaridhika tukasaini hati ya mauziano.
Lakini ndani ya mwezi mmoja tokea tumeuziana kwenye hilo eneo akaingia mwanamke kuishi kwenda kumuuliza anasema yeye ni mke wa aliyekuuzia hili eneo wakati anakuuzia mimi hakunishirikisha hivyo sitambui uuzwaji wa eneo hili na akiwa na yule mtoto.
Hebu wanajamvi naomba msaada hapo kisheria