Msaada wa kisheria kuhusu kuacha kazi

Msaada wa kisheria kuhusu kuacha kazi

h.imani

Senior Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
189
Reaction score
94
Mwezi wa Pili tarehe 10 niliandika barua ya kuacha kazi, notice ya siku 28, nilichokizoea na kukijua mimi ni kwamba mtu akiandika barua ya kuacha kazi then respond za majibu juu ya kuacha kazi zijibiwe.

Cha kushangaza hadi inafikia tarehe ya kuondoka nilikuwa sijajibiwa kukubaliwa either niache kazi ama hapana. Ila niliambiwa kwa mdomo kuwa kwakuwa tuko busy sana basi naomba uende halafu tutaindaa hiyo barua pamoja na mafao yako. Lakini cha kushangaza hadi hii leo sina document yoyote ile na mimi sipo kazini toka mwezi March.

Sasa siwezi kwenda hata NSSF kwenda kudai mafao yangu kwasababu sina barua ya mwajiri kama uthibitisho kuwa mimi sio mfanyakazi tena katika shirika hilo.

Je, kuna jambo lolote naweza kufanya juu yao kwamaana ya kuwashitaki? Au hakuna haja ya kupewa barua ya majibu ya barua yangu niliyoombea kuacha kazi?

NAOMBA MSAADA WENU TAFADHALI.
 
Back
Top Bottom