Ok mkuu ipo ivi, kuna jamaa alinunua eneo kwangu, akajenga na kumweka mke wake wapili aishi pale, baadae yule jamaa akaniomba eneo kidogo awe analima mboga mboga maana eneo lake lilikuwa ni dogo, sikuwa na hiana nikampatia alime kwa muda kisha nikilihitaji ntachukuwa tukakubaliana hivyo, kosa nililolifanya hatukukubaliana kwa mandishi. Basi siku zikaenda yule jamaa akafariki pale kwake akabaki bi mdogo,,,ndiye aliyeanza kuleta matatizo mara baada ya kuanza kujenga eneo ambalo mumewe aliniomba alime mbogamboga kwa muda, huyo mkewe anadi mukewe anadai mumewe alimwachia ni eneo lao, ikabidi niende serikalini ikiwa ni pamoja na mtendaji aliyehusika wakati wa kuuziana eneo, wakaja tukapima eneo kila kitu kikawa sawa. Baadae yule mke wa marehemu akatumia nguvu ya pesa na kwenda kufungua madai akilalamika ameonewa anapokonywa eneo, kama tujuavyo udhdaifu wa vyombo vyetu vilivyopewa dhamana ya kusimamia sehemu husika hudiliki kupindisha sheria kwa sababu ya pesa, basi kesi ikaenda mbele mpaka mahakamani..kwa kuwa kesi ipo mkoani nami nipo kuhangaika maisha yaendelee nikamtafuta wakili anisimamie hiyo kesi, pasipokuwa maskini kumbe ndo walewale wapigaji. Basi siku zikaenda hatimaye ndugu wa marehemu wakapata hizo taarifa na kumshauri yule mama achane na kesi aniombe msamaha na kuenda kufuta kesi mahakamani, alikubali kufanya hivyo lakini mpaka saizi kesi haijafutwa najaribu kuongea na wakili anasema natakiwa nimlipe kwanza yeye ndipo mambo yataenda mwisho, nimetupa gharama nyingi sana mbele ya haki yangu. Ndio sababu ya kuomba msaada wa kisheria humu jf, i hope ntasaidiwa asanteni.