WENYELE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,433
- 1,442
Ndugu zangu,mimi ni mmoja ya wazawa wa kanda ya Ziwa.Mwaka 2014 mwezi wa tatu nilitoa mahari kwa kulazimishwa kwa binti mmoja hivi aliyepata ujauzito wangu.Nilitoa ng'ombe 15,huyu binti skukaa naye ila aliniachia mtoto tu akarudi kwao.Nataka nirudishe ng'ombe zangu wakuu ila baba yake anazingua ili hali ana ng'ombe wangu.Nifuate njia gani za kisheria?