Msaada wa Kisheria kuhusu Mahari

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Ndugu zangu,mimi ni mmoja ya wazawa wa kanda ya Ziwa.Mwaka 2014 mwezi wa tatu nilitoa mahari kwa kulazimishwa kwa binti mmoja hivi aliyepata ujauzito wangu.Nilitoa ng'ombe 15,huyu binti skukaa naye ila aliniachia mtoto tu akarudi kwao.Nataka nirudishe ng'ombe zangu wakuu ila baba yake anazingua ili hali ana ng'ombe wangu.Nifuate njia gani za kisheria?
 
Achana nao hao ng'ombe maana mali zinatafutika wewe unafikiri nani anarudishaga mahari?
 
nenda mahakama ya mwanzo hapo kuna wazee wa baraza ambao wanajua fika mila za wasukuma watakusaidia kwa mujibu wa sheria na mila zenu. ila kumbuka kuwa yenu haikuwa ndoa kwani kuna kauli ya kulazimishwa ndoa ni hiari ya mke na mume.
 
Unatuaibisha wanaume. Think big.
 
Kuna dalili za kufunguliwa kesi ya kubaka japo hujataja umri wa msichana, ni hisia lakini nzito.
 
Ulitoa mahari kwa sababu gani kama mwanamke hukai naye?
 
Huo ujauzito ulimpa kwa kulazimishwa? Alirudi kwao kwa hiari au ulimfukuza maana kama ulimlipia mahari huyo ni mkeo ulipaswa kufuatilia kwa wakwe zako na kumrudisha kitandani kwako
 
bofya hapa kupata kitabu kinachoongelea yote hayo SHERIA TANZANIA
 
Achana nao hao ng'ombe maana mali zinatafutika wewe unafikiri nani anarudishaga mahari?

Hiyo ipo ya kurudisha, tena makabila mengine mwanamke hasiporudisha kuolewa tena hawezi au wazazi kupokea ya mwingine.

Na lama mwanamke ana mpango huo wanatafutaka sababu ex adai ili wawe free bila hivyo mila inampiga bao.

Kwa mleta mada ulizia wakubwa wako, fata wazee wa ukoo, ulizia mila na desturi za kwao ka kabila tofauti. Sema mtoto nae lazima ale.

Akitaka kurudi jua kasukumwa na nduguze ukachukua wanayofaidi na atachepuka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…