Mosi,
huyo amevunja haki yako ya faragha.(Right to privacy)
Katiba ya Tanzania katika Ibara ya 16 (1) inasema "Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi"
Pili,
amejifanya ni mtu mwingine kwa kupitia kompyuta.(Impersonation)
Hili ni kosa la kimtandao na adhabu yake ni milioni tano au miaka saba.
Ushauri wangu.
Mfuate muonye, akiendelea kukusumbua nenda polisi fungua jarada.