Msaada wa kisheria kuhusu ndoa ya Mengi na K-Lynn

Msaada wa kisheria kuhusu ndoa ya Mengi na K-Lynn

Van gaal

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2014
Posts
265
Reaction score
107
Ndoa ya leo ya Dr. Mengi na K-Lynn ni ya kweli? au ndio tusubiri siku Dr. Mengi ajekuita waandishi wa habari na kukanusha tena kuwa ni uvumi tuu?

Street is talking kwamba ndoa ya Dr. Mengi na mkewe Mercy is still valid (yani hawajatalikiana), kutokana na ukweli ya kwamba ndoa hiyo ilikuwa ni ya kanisa (until death do them apart). Sasa hapa ndipo ninapoomba msaada wa sheria katika maswali yafuatayo:-

1. Kama ni kweli ndoa ya kwanza haijatengulia, je Dr. Mengi atakuwa amevunja sheria ya inchi kufunga ndoa na K-Lynn hata kama ndoa imefungwa inchi nyingine?

2. Assume Dr. Mengi hakuweka wazi nani atakuwa muamuzi wake mkuu katika maswala ya afya. Je, kama ikatokea Dr. Mengi amepata matatizo ya kiafya na hawezi kufanya maamuzi muhimu, je inawezekana k-Lynn akawa na final say as it seems Dr. Mengi and his first wife doesn't get along?

3. Kwakuwa K-Lynn anawatoto na Mr. Mengi, je hao watoto watakuwa part of Mengi's estate hataka ndoa hiyo ikagundulika kuwa batili?

4. Kama mke mkubwa akajatambua kwamba kweli kuna ndoa imefungwa wakati yeye bado ana ndoa halali na Dr. Mengi, je, kisheria naruhusiwa kumfikisha Dr. mengi mahakamani na kumshitaki?

Naomba mtusaidie kujua atamshitaki kwa kutumia kipengele kipi cha sheria?

Asanteni!

kifungu cha 11 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971....kimeruhusu kubadilisha ndoa kutoka ya mke mmoja kwenda wake wengi endapo wanandoa watakubaliana...nenda kasome hiko kipengele Van gaal
 
Last edited by a moderator:
Kwa inavyosema sheria ya ndoa mtu akiwa bado yuko kwny ndoa halalo ya kikristo haruhusiwi kuoa mwanamke mwingne na ikitokea kaoa hiyo ndoa ya pili ni batili hata watoto walio zaliwa kwny hiyo ndoa ya pili ni batili na hawana chochote kwny urithi wa baba yao
Na kuhusu suala la nan mwny maamuzi sahihi juu ya afya hilo pia linarudi kwa mke halali wa mhusika mwenyewe
Na kuhusu suala la kumfikisha mahakamani ikiwa ataja gundua kuwa kaoa iyo pia m/ke ana haki hiyo kumshitaki ata yule muolewa kwa kuingilia agano lao na haki yao ya kindoa (consortum right) na kuwashitaki kwa ugoni
 
Watanzania bwana,ili iweje sasa.

Sioni umuhimu wa kujadili hi post humu, kwanza inakiuka privacy ya mtu, na haileti mafundisho yoyote hapa, kwanza kumbuk mzee mengi ni msomi, na anamwanasheria wake bw michael ngalo, huyu ni mshaur wa maswala yote ya kisheria juu ya mzee na kampuni. Hakuna kilichovunjwa hapo, by the way naomba tujadili vitu vyenye tija kwa hili halituhusu.
 
Mambo ya kanisa hayapo kwenye katiba

mke mmoja, mme mmoja ni mambo ya madhahuni

Yawezekana Mengi Ameasi kanisa .....hana makosa

kama ambavyo mkristo aweza badili din na pia mwislam aweza badili din.

wote wako above 18yrs na akili timam. Nimaamuzi yao.
 
ndiyo maana tunasema dini ni uislam,utata huo usingekuepo Mengi ana wake wawili kwa sasa,labda kama Mengi ameukana ukristo

Sheria ya ndoa haimlazimishi mtu kuendelea kuishi na mke au mme ambaye hamfai hivyo hurusu watu kutengana kwa talaka na kuoa au kuolewa kwingne.
Pia mtu anaruhusiwa kufunga ndoa ambayo itamruhusu kuoa mke mwingne (semi-poligamy mariage).
Sioni tatizo kwa hili mtu kuoa mwingne japo si muislam
 
Mambo ya kanisa hayapo kwenye katiba

mke mmoja, mme mmoja ni mambo ya madhahuni

Yawezekana Mengi Ameasi kanisa .....hana makosa

kama ambavyo mkristo aweza badili din na pia mwislam aweza badili din.

wote wako above 18yrs na akili timam. Nimaamuzi yao.

Suala sio above 18 kifungu cha 9(1) cha sheria ya ndoa kinasema ndoa ya kikriato ni ya mme1 na mke1 kwaiyo kuwa na miaka 18 pekee hakuifanyi ndoa kuwa halali
 
Jamani muwe mnasoma maandiko na kuyaekewa hii ya kusoma mstari mmoja wa biblia na jump on conclusion inatiasha sana ukristo wenu na kubaki kuhukumu wengine.

Ukisoma kitabu cha Biblia Mathayo 19: 3-9

3 Na Mafarisayo wakamjia, wakikusudia
kumjaribu na kusema: “Je, ni
halali mwanamume kumtaliki
mke wake kwa kila
sababu?”

4 Akajibu, akasema: “Je, hamkusoma kwamba yeye aliyewaumba hao kutoka mwanzo aliwafanya mwanamume na mwanamke,

5 na kusema, ‘Kwa sababu hiyo
mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’?

6 Hivi kwamba wao si wawili
tena, bali mwili mmoja. Kwa
hiyo, kile ambacho Mungu
ameunganisha mtu yeyote
asikitenganishe.”
 
Huo ulikuwa mtazamo wa kikatoliki ambao hadi kesho hawatambui talaka lakini yalipoanzishwa makanisa ya kipasta (pastoral church) walikubali talaka na kusema si jambo la kibinadam wala kiroho kumlazimisha mtu kuendelea na mtu ambaye hamfai.
Chukulia mfano mtu kaolewa na mtu ambaye kila kuchao ni kupigwa tu, kutishiwa usalama wake wa kuishi bado hiyo mistari uloitoa utaisimamia ili kupotezea uhai?
 
3 Basi Mafarisayo
wakamwendea, wakamjaribu,
wakimwambia, Je! Ni halali
mtu kumwacha mkewe kwa
kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia,
Hamkusoma ya kwamba yeye
aliyewaumba mwanzo,
aliwaumba mtu mume na mtu
mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo,
mtu atamwacha babaye na
mamaye, ataambatana na
mkewe; na hao wawili
watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili
tena, bali mwili mmoja. Basi
aliowaunganisha Mungu,
mwanadamu
asiwatenganishe.
7 Wakamwambia, Jinsi gani
basi Musa aliamuru kumpa
hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa
sababu ya ugumu wa mioyo
yenu, aliwapa ruhusa
kuwaacha wake zenu; lakini
tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila
mtu atakayemwacha mkewe,
isipokuwa ni kwa sababu ya
uasherati, akaoa mwingine,
azini; naye amwoaye yule
aliyeachwa azini.
 
Back
Top Bottom