Msaada wa kisheria kuhusu suala hili la mirathi

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,475
Habari wadau,

Naomba msaada wa kisheria kuhusu mirathi. Mwanzoni mwa mwaka huu Baba yangu mzazi alistaafu , miezi kadhaa baada kustaafu alipata ajali ya Gari na kufariki siku chache akiwa hospital.

Kutokana na kwamba Baba yetu alikuwa mstaafu tulianza taratibu za kufuatilia mirathi hasa hela zilizopo kweny account yake ya NMB.

Tulifuata taratibu zote za kisheria mpaaka tukamaliza lakini shida imekuja kwa hakimu anayeisimamia kesi yetu yeye yupo likizo na karani wake anasema tusuburi mpk arudi likizo mwezi ujao ndo amilizie kutia sign ili fedha ziingizwe kwenye account zetu.. tumejaribu kupambana lakini mpk sas hakuna matumaini ya kupata hizo fedha na mtaani tuna madeni tulitegemea kupata hzo fedha ili kulipa hayo madeni.

Kwa jinsi inavyoonekana kuna mianya ya rushwa inatengenezwa. Naomba msaada nifanye nini ili kupata haki yangu bila kutoa rushwa.
 
Mnaweza mkatumia pesa nyingi kuliko mnayoidai.

Hii mikopo ni njia mojawapo pia ya kuwanyonya wafanyakazi.

Mara nyingi mfanyakazi huwa anaweka mikopo yake sawa ili atakapostaafu asikatwe kiinua mgongo chake kulipa mkopo.

Shida kubwa pia hapo unaposema kuwa mkopo ulikuwa na bima.

Hiyo bima ni kubwa kiasi gani ya kufidia mkopo wote.

Pia wakati mtu anakopa kuna next of kin unamwandika ili likitojea la kutokea alipe mkopo,

labda vile mzee alikuwa mwajiriwa ajira ndo ilimbeba au ndo was next of kin, sijui.

All in all kwa nji hii ninayoijua mie you may waste time and money na mkaambulia patupu.

Hili tatizo la watoto wetu, they're here waiting ukufe wale mafao.

God took his person, ndo mparagane kusaka zenu.

Sorry for this hard message.
 
Kuanzia mwanzo kabisa mlikuwa na huyo hakimu?

Kama mlikuwa naye na ameenda likizo tatizo liko wapi hapo mpaka unahitaji msaada wa kisheria? Ninavyojua ni kweli jalada halitakiwi kwenda kwa hakimu mwingine, inabidi huyo aliyeko likizo arudi ndio atie saini.

Mkifosi mwingine atie saini documents zenu zinaweza zikakataliwa huko mbele, kuweni makini sana msiwe na haraka sana mambo ya pesa hayahitaji pupa.
Unforgetable
 
Yes msaada wa kisheria niliuhitaji ili kujua kam hakimu akiwa likizo mwingine hawezi kufanya kazi yake
Kama ni kweli ulivyosema bac tayar umenisaidai mana ckuwa nafaham before kama Sheria ipo hvyo [emoji120]
 
Ebu soma vzr thread yangu
Hakuna sehem nimesema kuwa mzaz wangu alichukua mkopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…