Emmado
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 225
- 276
Ndugu wadau!
Kuna mwanamke mmoja nilishawahi kuwa nae kimapenzi na baadae bahati akapata mimba, tukapata mtoto mmoja. nikajaribu kumweka ndani awe mke wangu, tulikaa miaka miwili pamoja, alikua na matatizo madogo madogo ya kitabia nikajaribu kurekebisha ikawa tabu ilipofika mwaka wa tatu mwishoni akaniambia amenichoka akaondoka na kila kilichokuwa chake.
Nilimbembeleza sana afikirie mara mbili ikashindikana, nikamshauri aniachie mtoto nimsomeshe akagoma ila baadae nikampeleka ustawi wa jamii ikaamuliwa anipe mtoto kwa ajili ya shule.
Tangia hapo nikawa nimepumzika rasmi kwa miaka mitatu, sasa tatizo limekuja juzi baada ya kusikia nataka kuoa akaanza kunitumia sms za ajabu ajabu ila ya mwisho akaniambia hawezi kuniacha nikaoa labda afe.
Sina tatizo sana na vitisho vyake ila;-
1} Je endapo akiamua kuja kuzuia ndoa yangu kwa pingamizi je atakuwa na nguvu kisheria
2] Naweza pata kinga ya kisheria ili hili lisitokee?
3] Nifanyeje asiniharibie tukio langu la kihistoria?
Naombeni msaada wadau!