Msaada wa kisheria kupata wakili wa serikali

Ngosi

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
390
Reaction score
189
Habar wana jf?
Naombeni msaada wa kuweza kupata wakili wa serikali, maanake kuna kaka yangu amekamatwa tangu januari mwaka jana 2012 hadi leo yupo gerezani na bado ni mahabusu. Amekamatwa kwa kosa la jinai (criminal cases) na anashitakiwa na Jamhuri, kesi haina mlalamikaji wala shahidi sema ametuhumiwa. Ndugu tumejitahidi kumuwekea dhamana wamekataa na polisi wanataka mil 4 na sisi hatuna
 
katika criminal case, kama kesi imefunguliwa mahakama kuanzia ya wilaya kwenda juu, hauwezi kumwona mlalamikaji akaja pale ikiwa na maana ya victim wa ile crime, bali mlalamikaji wake huwa ni jamhuri(ikiwakilishwa na wakili wa serikali au public prosecutor mwenye mamlaka aliyopewa na dpp). hivyo, katika kesi yako kama iko mahakama ya wilaya, mlalamikaji ni huyo mwendesha mashitaka, victim atakuja tu kama shahidi. makosa ya jinai yaani yale ambayo raia anafanya jinai dhidi ya raia mwingine, kwasababu katiba ya nchi inaipa serikali wajibu wa kuwalinda watz wote, basi ukimfanyia jinai raia serikali inao wajibu kumlinda, yaani kukushitaki badala yake yeye, hivyo jinai dhidi ya raia ni jinai dhidi ya serikali na wakili wa serikali/public prosecutor atakushitaki (wakimuwakilisha dpp). mawakili wa serikali wapo kila mkoa kwa sasa, uliza katika kila makao makuu ya mkoa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ipo wapi, watakuonyesha, ukienda polisi kuuliza hao lazima watakuonyesha kwasababu sik,u hizi polisi wakikamata mtu hawaandai hati ya mashitaka lazima wapeleke jalada ofisi ya mwanasheria mkuu wakaandae na kupeleka mahakamani, polisi wanapeleka mahakamani watuhumiwa tu (katika maeneo yale ambayo ofisi ya mwanasheria mkuu imefunguliwa).

wakati mwingine, hatujui ni kosa gani ndugu yako anashitakiwa nalo, ungetuambia tungejua na kukushauri, lakini maadamu ni bailable(umesema polisi wanataka rushwa), naamini ukitimiza vigezo ataweza kupata dhamana. polisi hawana mamlaka kutoa dhamana kwa mtu pale ambapo atakuwa ameshafikishwa mahakamani, limit ya uwezo wao kutoa dhamana ni pale tu ambapo suspect amekamatwa tu hajafikishwa mahakamani bado, akifikishwa mahakamani tu ndani ya masaa 24 (au zaidi kama kuna sababu maalumu), mamlaka yote haiko kwao tena, bali mahakama ndiyo yenye mamlaka kutoa dhamana au la, na huweka conditions ambazo wakili wa serikali/mwendesha mashitaka pia anaweza kupinga kama ataona mahakama inaenda kinyume na sheria, ila mahakama ndiyo yenye mamlaka.

wakati mwingine kesi inaweza kuchukua mda mrefu kwasababu ya nature ya upelelezi. ukitoa hizo hela polisi watakulia hela bure na hawawezi kukusaidia. wanaweza kukudanganya kuwa izo hela utakazotoa wataenda kuwahonga mahakmimu etc, lakini niwajuavyo polisi watazila na hutafanikiwa. tuambie kosa alilotenda, ipo mahakama gani, na amepewa conditions gani za bail/dhamana ili tukushauri vizuri. hapa ndani kuna mawakili wa serikali wengi tu, utapata majibu.
 
Kwa kuongezea kwenye Maelezo ya liyotolewa na mdau hapa chini ni kwamba, kwanza elewa mawakili wa serikali huwa hawatoi uwakilishi mahakamani kwa watu binfsi isipokua kwa serikali tu (to avoid conflit of interest) kwa mtu binafsi (mshitakiwa) atapewa uwakilishi na private Advocate(wakili wa kujitegemea) mawakili hawa itabidi ulipie gharama za uwakilishi wao ila kwa kesi ambazo ziko mahakama kuu na zinazoushisha adhabu kubwa (capital punshment) mfn Mauaji, mawakili wa kujitegemea utoa msaada(pro bono) wa uwakilishi bure kwa watuhumiwa wa makosa hayo wasiokuwa na uwezo wa kuweka mawakili, sheria na kanuni za kazi yao zinawataka kufanya hivyo.
sasa kwa kuwa hujasema kesi ya huyo ndugu yako inahusisha kosa lipi na hiko mahakama hipi natumaini utaweza kuelewa kupitia maelezo hayo machache ya kuhusu uwakilishi wa wanasheria.
Kucheleshwa kwa shauli lako, nijuavyo mimi na sheria inavyosema, mtuhumiwa yeyote aliyopo mahabusu anatakiwa kila ndani ya siku 14 hawe ameletwa mahakamani kusikiliza shauli lake, na amini hilo ndio linalofanyika kwa ndugu yako na pale apofikishwa mahakamani ulezwa na mahakama shauli lake limefikia hatu gani na nini kinafanyika, mfano upelelezi haujakamilika kwahiyo linapangiwa tarehe nyingine, na kama mtuhumiwa haridhiki na mwenendo wa shauli lake anayo haki ya kuhoji nini kinakwamisha na pengine kuiomba mahakama itupilie mbali shauli hiyo kwa kua upande wa mashitaka wameshindwa shindwa kuendeleza shauli (want of prosecution).
Kuhusu dhamana kama alivyosema mdau Mshpacha Brucha, shauli likisha pelekwa mahakamani, mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kutoa dhamana na sio polisi iyo milioni unayoombwa unapigwa tu hamana kitu, na dhamana ni haki ya mtuhumiwa na ni lazima kama kosa la mshitakiwa linadhaminika hakimu au jaji amueleze mtuhumiwa anayohaki ya dhamana na atamueleza vigezo vya dhamana yake, na ka hajamueleza hilo mtuhumiwa pia anaweza kuihoji mahakama kama inawezampatia dhamana.
Inatuwia vigumu kukupa ushauri mzuri maana hata maelezo yako mdau Ngosi hajakamilika, hajulikani nini kosa la kaka ako na ameshitakiwa katika mahakama hipi nikimaanisha ya Wilaya/hakimu mkazi au mahakama kuu ila akili yangu inanituma niamini ni mahakana za chini ya mahakama kuu.
Pole kwa matatizo mdau; mahakama itatenda haki kadri ya sheria inavyotaka na haki itaonekana imetendeka.

 
kimsingi nakubaliana na maelezo ya Mbeki hapo juu, nafikiri kujua jina la mahakama siyo issue, pili ni kwamba kikubwa ni kujua kosa gani, na ni level gani ya mahakama. pia ni vizuri kuweka wazi kwamba kwa sababu High court inasikiliza kesi zilizoanza kwa committal proceedings then as a matter of logic itakuwa iko katika subordinate court.Then kama anaona hiyo confinement haiko proper then unaweza omba writ ya habeous corpus, ni rahisi tuu. kwa leo ni hilo tuu









:majani7:
 

Jamani wanasheria na kilatini chao! Sasa writ ya Habeous Corpus, mwenzako ameelewa nini?!! Ha, just a joke ndugu.
Nyongeza katika hili kumsaidia mwenzetu ni kwamba kama amenyimwa mdhamana bila sababu yoyote au bila kueleza sababu, hii kwa sisi wanasheria tunaweza kusema, haki ya mtuhumiwa ya Ibara ya 18 aya (d) yA Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, imevunjwa. Pili kumnyima mtu mdhamana ni kumtia mtu hatiani tayari ambapo si mdhamana tena unohitajika ila, labda, msamaha. Kwasababu jamaa yako hajahukumiwa, kumnyima mdhamana ni kuvunja haki yake ya kikatiba Ibara ya 13 ibara ndogo ya (6) aya (b) ambayo inamlinda mtuhumiwa under principle of presumption of innocence. Lakini kama kosa alilotenda ni kati ya yale yaliyotajwa katika kifungu cha 148 kifungu kidogo cha (5) (a) cha Sheria ya Uendeshaji wa Makosa ya Jina iliofanyiwa mapitio 2002, hatopata mdhamana. Pili endapo DPP atakuwa ameitaarifu mahakama kuwa kumwacha kwa mdhamana mtuhumiwa huyo kunaweza kuhatarisha usalama au haki ya Jamuhuri. Kama vigezo hivi havihusiani na kosa alofanya jamaa yako, kata rufaa mahakama ya juu,
 
Very well said learned bro! unajua wakati mwingine pia, hatuambii ni kosa gani amefanya huyo ndugu yako hata akawa ndani muda wote huo. mtu akisomewa tu charge mahakamani kwa mara ya kwanza, kama kosa linadhaminika, huwa anaambiwa na mahakama kuwa anayo haki ya kupata dhamana, na anaambiwa palepale masharti ya kutimiza dhamana. kuna uwezekano wakati mwingine kosa likawa halidhaminiki, halina dhamana hadi pengine aende High court, mfano makosa yote yaliyoko kwenye cap.200 yaani Economic and Organized Crime Control Act, makosa yote ya Economic crime offences (uhujumu uchumi) hayana dhamana subordinate courts hadi mtu aende kuomba dhamana kwenye High court. makosa yote ya human trafficking, makosa yote kwenye national security Act, na wakati mwingine dpp anaweza kuwa ameweka certificate kwenye makosa fulanifulani akizuia dhamana kwa maslahi ya umma etc. hivyo angetuambia kuwa huyu ndugu ametuhumiwa kosa gani, hapo tungemshauri kulingana na kosa lenyewe na mahakama yenye uwezo kutoa dhamana hiyo. mashitaka mengi huanzia subordinate courts including those of committal proceedings na yale ya kawaida, na sio rahisi, kama hakuna sababu ya msingi, akawa yuko ndani hadi leo.

huyo polisi anayeomba rushwa kuna uwezekano akawa anamdanganya kuwa akimpa hiyo rushwa ataenda kuongea na hakimu pamoja na waendesha mashitaka/mawakili wa serikali etc, ili pengine charge ibadilishwe etc, tuna guess tu vitu vyote kwasababu hatujui kosa gani ameshitakiwa nalo. ila kama ni kosa bailable, anastahili dhamana na dhamana itakuwa wazi, afuate masharti tu ili ndugu yake apate dhamana. kama kwenye mahakama aliyopo kosa halidhaminiki, basi, aende kwenye mahakama husika eg.high court. kama ni murder case, hiyo haina dhamana kabisa, hata treason pia. soma s. 148 CPA, pia soma sheria zingine za makosa hayo niliyoeleza hapo juu. poleni.
 
asante kwa nyongeza nzuri ila nitoutiane kidogo na hoja yako ya pili.natambua haikuwa kesi ya kwanza kueleza hivyo ila ile kesi ya Daudi pete mahakama ilikataa tafsiri kwamba kumnyima mtu bail basi ni kumchukulia kama convict tayari.kwa sababu kila jambo lina wakati wake labda tukutane tena hapa katika muda mwafaka, big up bro
 

Asante mkuu. Kwenye kesi ya Daud s/o Pete v R, issue ambayo court ilikuwa inajaribu ku-determine ilikuwa kutoa tafsiri sahii ya Ibara ya 18 ya URT Constitution under presumption of innocence, hivyo Mahakama ikawa ina-construe kama kumnyima mtu dhamana ni sawa na kum-treat kama convict kwa lengo la ku-evaluate the constitutionality of the Statutes zinazo weka exceptions ktk grant of bail kama section 148 ya C.P.A nitarudi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…