Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,986
- 5,058
Nina mpwa wangu kaolewa miaka mitano iliyopita. Kabla ya kuolewa alikuwa mfanyabiashara, na alipoolewa mumewe akamwambia afunge biashara yake wawe wanafanya pamoja akakubali.
Baada ya muda mumewe akaanza kumzuia kuingia dukani na kuweka wafanyakazi wa kuuza. Mke alipomuuliza aliishia kumfokea tuu na kumwambia ndugu zake wamemwambia anaiba hela. Baadaye akamwambia akae tuu nyumbani yeye si mwanamke?
Kinachosumbua ni kwamba sasa hivi hata nguo hamnunulii, vocha ndugu zake ndio wanamnunulia na mwanaume anaweza kuondoka bila kuaga zaidi ya miezi mitatu na asipige simu.
Alipoongea na ndugu wa upande wa kiume walimjibu vibaya kiasi cha kutaka kuondoka lakini hakuweza kufanya hivyo kwani wana watoto.
Kilichonifanya kuomba ushauri;
Ndugu zake tunataka kumpa mtaji ili afungue biashara yake ambayo itamsaidia kwenye mahitaji yake madogo madogo kwani hajazoea kukaa nyumbani.
Pia uhakika wa uhai wa mtu ni mdogo sana na mumewe anaweza kufa muda wowote mpwa akashindwa pa kuanzia kwani tuna uhakika ataporwa mali zote(japokuwa anaweza kutangulia yeye).
Ni taratibu zipi za kisheria au kijamii za kufuata?
Tukifanya hivyo ni kosa gani tutakuwa tumefanya?
Nitashukuru kama nitapewa na njia sahihi ya kupita.